ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 23, 2010

mazishi ya Ndugu yetu Amour Hemed Ally(Abraham Allen),Sept 23,2010,Harrisburg PA


SHUKURANI

Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake(New York Metro Tanzanians Community)inatoa shukrani zake za dhati kwa wale wote walioshiriki katika kufanikisha mazishi ya ndugu yetu Amour Hemed Ally(Abraham Allen)yaliyofanyika jana Sept 23,2010 kule Harrisburg PA.
Shukurani maalum ziwaendee kwanza viongozi wa jumuiya ya waislam ya Washington(TAMCO)kwa wepesi wao wa kufikiri kwa uratibu wa Bwana Mganga Muhombolage akishirikiana na bwana Yacob Kinyemi.Ahsante yetu kwa wanachama wote wa jumuiya hii na tuendelee kushirikiana.
Pili shukurani maalum ziuendee ubalozi wetu pale Washington DC kwa ushirikiano wao mkubwa waliouonyesha ukiongozwa na Muheshimiwa Balozi Maajar na ufuatiliaji wa karibu kabisa wa bwana Abbas Misana.Tumefarijika sana na misaada na ushirikiano wenu mliotuonyesha.Ahsante yetu kwa wafanyakazi wote wa ubalozini kwa michango na mawazo yenu.
Tatu shukurani maalum kwa Balozi zetu pale Umoja wa Mataifa New York kwa ufuatiliaji wenu wa karibu pamoja na michango kutoka kwa wafanyakazi wa ubalozi iliyofanikisha kwa kiasi kikubwa katika ukamilifu wa msiba huu.Ahsante sana Balozi Sefue,Mama Steiner na wafanyakazi wote wa ubalozini.
Nne shukurani maalum kwa jumuiya za Watanzania zilizojitokeza na kutusaidia aidha kimawazo ama kwa salamu zao za Rambirambi.Ahsanteni viongozi wa jumuiya za California na Washington Seattle Kwa mioyo yenu.
Mwisho shukurani maalum kwa viongozi wenzangu wa jumuiya yetu ya New York Metropolitan Tanzanians Community kwa uwezo wenu mkubwa mliouonyesha katika kukamilisha msiba huu.Ahsanteni sana Bwana Michael Chiume,Shabani Mseba,Amiri Kius,Mama Kiswaga,Bi Asya Mwilima pamoja na wanajumuiya wote.(Sheikh Masoud Maftah,Yussuf na Bwana Tahir Bilal Ahsanteni sana).

AHSANTENI SANA
INTERIM CHAIRMAN,HAJJI KHAMIS. 

No comments: