ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 11, 2010

Watoto walindwe


Nimka akiwa katika jukwaa la siasa akiwa anautubia na kutoa sera mbalimbali ambazo wananchi wanatakiwa kuzifuata ilikueupa kuwanyanya watoto pamoja na kukemea ukatili dhidi ya watoto nchini.
JAMII na mamlaka husika zimetakiwa kuchukua hatua ya haraka ya kuhakikisha inawalinda watoto ilikuepuka matatizo mbalimbali ikiwemo vitendo vya kilaghai na ukatili vinavyofanywa na watu wasio jali hutu wa watoto.
Nimka akionekana akigawa maji kwa umoja wa watoto waishio  mazingira magumu wanaoitwa ;New Hope Family Street Children' ambapo akifanya moja ya kazi zake za uharakati kwa watoto
Akiongea na .......jana .....jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea Haki za Watoto nchini, Nimka Lameck (11) alisema kipindi hichi kumekuwapo na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wadogo huku jamii ikinyamaza.
Nimka alizitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwalinda watoto waliohitimu elimu ya shule za msingi hivi karibuni hususan watoto wa kike ambao kwa asilimia kubwa wapo hatarini kushawishika na walaghai hao  maafu kama ‘Mafataki’.
“Watoto wanahitaji kuangaliwa kwa umakini na kulindwa kuepuka matatizo ya kutendewa mahovu kwa jamii isiyo na hutu wa watoto wadogo ambao wanakatisha ustawi wa watoto nchini” alisema Nimka.
Alitoa wito kwa wazazi kuwa na mwamko wa kuchunguza mienendo ya watoto wao mara kwa mara ikiwemo kuwakataza tabia hatarishi ambazo wanaweza kukumbana nazo kipindi wawapo majumbani.
Katika nyingine, Nimka alikemea na kurahani vitendo vya kikatili vilivyolipotiwa kwenye vyombo vya habari juu ya watoto wadogo kuwawa kikatili ikiwemo na kubakwa vilivyofanywa na watu wazima.
“Vitendo vilivyolipotiwa vimesikitisha,vimetikisa watoto wengi si wa Tanzania tu, bali hata dunianikote kwani watoto waliotendewa unyama huo walikuwa hawana hatia tunaomba sheria kali dhidi ya wahusika” alisema Nimka.
Aidha, alisema kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho kuandaa mpango maalum juu ya kutoa changamoto kwa watoto hapa nchini utakaoitwa ‘Haki Mtoto’.

No comments: