Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Jaji Damian Lubuva amtangaza Dk. John Pombe Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote na kumshinda mpinzania wake mkuu Ndugu Edwarld Lowasa aliyekuwa anagombea kwa tiketi ya Chadema kupitia muungano wa vyama vinne vya upinzani UKAWA, Dk John Pombe Magufuli ameshinda kwa kura 8.882.935 sawa na asilimia 58.46 huku Edwarld Lowasa akipata kura 6.072.848 sawa na asilimia 39.97.
10 comments:
Ndo tUnataka akachape kaazi sasa maneno Mengi hatutakiiiiii!!! Tunamtuma Ikulu kubadilisha mfumo mbovuuuuu uliopo hivi sasa!!!! Maneno Mengi hatuyataki hakika! Mungu ibariki Tanzania....
Viva maendeleo Tanzania. Hii habari haikuanzia kwenye kampeni hadi uchaguzi! Tangubkuanza kuandikishwa wapiga kura kwenye daftari ilikuwa ni mizengwe tupu. Na hivyo viashiria ndivyo vilivyokuwa na daftari B hivyo waTanzania waliingia kwenye uchaguzi bila kujua kwamba NEC ilishaanza kupiga kura ndani kwa ndani. Tunasubiri neema ya maji, umeme, barabara, chenji kibao kwenye mifuko millioni 50 kila kijiji na viwanda lukuki tuoloe ajira. Mungu bariki WaTanzania kuwaondolea upumbavu na umasikini.
Hongera sana na wate tuliokupa kura zetu tunakupongeza sasa kilichobaki ukiingiaa tuu Ikulu uza mpaka wale sisimizi ukimaliza wanyama wote ruksa msimamo ni ule ule
50+5=super ujima
Not that fast. Ushindi wa wizi ni wenu wenyewe. Wapenda mabadiliko sisi hatuwatambui. Sasa ndio ccm inaichafua Tanzania. Hakikubaliki kitu hapa.
Hahahaaaaaa wamejipatia tena miaka mingine 5 ya kuoga na ndoo na kuwasha koroboi lovely
Hongera sana Magufuli, Lowasa alianza kutumia njia ya rushwa kuingia ikulu akiwa angali CCM kwa kuwanunua watu muhimu ndani ya chama hicho na aliendelea kutoa rushwa na hongo katika kujipatia nafasi ya kugombea uraisi chadema kimabavu na hivi sasa baada ya kushindwa uchaguzi anataka kutumia mabavu kujiingiza ikulu kwa kutoa visingizio vilisivyokuwa na mshiko wowote na chengine tunachokijua lowasa lazima atakimbia nchi na nnaimani vyombo usalama vitakuwa karibu nae yule mzee anamengi ya kujibu baada ya mahakama ya ufisadi kuanzishwa na nafikiri itakuwa busara kama atanyang'anya pasi yake ya kusafiria asije akatoroka maana anajua kwa magufuli lazima sheria itachukua mkondo wake.
Imekula kwenu wachumia tumbo! Watanzania ningewashangaa sana kama wangeikabidhi nchi yao kwa fisadi papa na genge lake la vibaka wa Kanda ya Kaskazini. You should use your brain, even for just half a day! How can someone who spends billions of shillings to win a presidential election put your interest, instead of his financiers' interest, first? Do you know who provided that whopping financial support?
Mengi yatasemwa lakini mwisho wake ni kimya kizito kitatawala. Kama upinzani wataendelea kushabikia matusi tu na malalamiko yasiyo na mwisho badala ya kukaa na kujiuliza wapi wanakosea na hivyo kutafuta ufumbuzi wa makosa yao nina uhakika kabisa kuwa kamwe hawata shika uongozi wa nchi yetu.
Dua za kuku.Magufuli ndio raisi wa Tanzania, hutaki the country next door ( south Sudan) bado wanahitaji raia.
Post a Comment