NI Miss Tanzania 2006, Wema Abraham Sepetu ameibuka tena, safari hii picha zake akiwa katika pozi la kimahaba na njemba moja nchini Marekani zimenaswa.
Picha hizo zaidi ya tano zinamuonesha Wema na mwanaume huyo wakiwa ‘klozdi’ ambapo ‘mpelelezi’ wetu anamtaja jamaa kwa jina la Paul Masoud, ambaye ni Mtanzania aliyepiga kambi mji wa Boston nchini humo.
Ukweli ulio wazi mlimwende huyo anayejiita mke wa mwanamuziki Chalz Baba wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ yuko Marekani kwa sasa ambako alikutana na Masoud anayetajwa kuwa na mke na mtoto mmoja.
Mazingira ya wawili hao kukutana na kupiga picha za kichokozi yalikuwa na giza jambo lililosukuma ari ya Gazeti hili maarufu kwa kutoficha siri za mastaa wa Bongo kuingia kazini kupembua ‘mchele.’
Ilikuwa Septemba 19, 2010 Jumapili mchana, Masoud ‘alipandiwa hewani’ na Mwandishi Wetu kwa namba zake +17815266…, lakini mara zote simu yake ilitoa ujumbe wa kuongea ukimtaka mpigaji kuacha meseji kwa sauti (Voice Mail).

Asubuhi na mapema Septemba 20, 2010 Jumatatu, saa 12:56, Masoud alimtwangia simu Mwandishi Wetu na kumsalimia kwa ‘Kimombo’ (Kiingereza) ambapo Paparazi naye alimjibu kwa lugha hiyo hiyo, lakini akamtaka wakienzi Kiswahili kwa sababu anajua yeye ni Mbongo halisi.
Baada ya Masoud kusikia ‘amri’ hiyo alimsabahi Mwandishi kwa kusema; “mambo vipi?” Mazungumzo yalianza akijulishwa habari ya picha kwa mapana na marefu.
Masoud: Kweli Wema namfahamu, lakini ni dada yangu, na kama ni picha sijapiga naye.
Amani: Kwa hiyo hizi picha nilizonazo si zako?
Masoud: We unaishi ulimwengu gani bwana, hujui siku hizi watu wanatengeneza picha?
Amani: Kwanini wakutengenezee wewe na Wema na asiwe mtu mwingine?
Masoud: Swali hilo linataka muda kulijibu, nipe muda.
Amani: Halafu tunasikia una mke na watoto wawili na umekorofishana na mkeo kwa sababu ya W…
Masoud: Mbona wewe unaongea kama upo hapa hapa Marekani? Mimi nina mke na mtoto mmoja wa kiume na sijakorofishana na mke wangu.
Amani: Kwa hiyo kuhusu picha?
Masoud: Hilo nimeshajibu.
Mazungumzo kati ya Masoud na Mwandishi yalichukua dakika 8 na sekunde 27 akisisitiza Wema ni dada yake.
Habari za ‘kipelelezi’ zinaweka wazi kuwa, Jumatatu hiyo hiyo, mwanaume mmoja jijini Dar (jina tunalo) alimpigia simu mama Wema na kumuuliza kuhusu Paul Masoud ambapo alikiri kumfahamu.
Lakini kama kawaida yake mwanamama huyo kabla ya kufafanua zaidi alitaka kujua sababu za yeye kuulizwa, alipojibiwa kuwa ni mambo yanayohusu habari aliwaka na kuongeza:
“Huyu kijana kakulia hapa mtaani Sinza Mori, ila kwa sasa anaishi Marekani na ni rafiki wa familia ya Sepetu lakini hakuna kingine.”
Aidha baada ya mama huyo kupika mchanyato wake wa habari, Saa 12:26 jioni ya siku hiyo hiyo, Wema alimwendea ‘angani’ Mwandishi Wetu na kutoa ufafanuzi ufuatao:
“Masoud ni family Friend wetu, naweza kusema amenilea kwani tumekuwa naye mtaani Sinza tangu mimi nikiwa mdogo, nimekuja huku kwa dada’angu nimekutana naye.
“Suala la kupiga picha si ajabu…mimi napenda picha ndiyo maana huwa wakati mwingine najipiga mwenyewe,” alisema Wema.
Aidha dakika za mazungumzo ya mwandishi na Wema zilipozididi kukatika iliibuliwa hoja kwamba Masoud aliyekiri kumfahamu Wema na kukana kupiga picha naye alipozungumza na mwandishi ni mwingine.
“Aaa..we si unasema umeongea na Masoud asubuhi, mbona mimi nimemuuliza kasema hajaongea na mwandishi yeyote asubuhi…ngoja umsikie mwenyewe,” alisema Wema huku akimuunganisha mwandhishi kwenye mazungumzo ya pamoja ya njia ya simu (conference).
Katika mazungumzo hayo mtu aliyeitwa kwa jina hilo alikana kuongea na Paparazzi wetu hata pale aliposomewa namba zake na Wema aliyekuwa mwenyekiti wa mjadala aliingiwa kirusi na kuanza kuporomosha matusi ya nguoni.
Baada ya hali ya hewa kuchafuka, dada yake mnyange huyo ambaye wakati wote wa mazungumzo hakujitambulisha jina aliingilia kati na kuomba mdogo wake aachwe apumzike.
Kujieleza kwa Wema na matusi yake, dada mtu na Masoud ‘wao’ kulitumia dakika 12 na sekunde 18.
Kutoka mezani kwa Mhariri: Kilichotakiwa kutoka kwa Wema ni ufafanuzi wa picha na uhusiano wake na Masoud na si vinginevyo. Matusi hayakuwa na sababu, kwani hakuambiwa alikuwa na mpenzi mpya wala hakuambiwa ni kwa nini alipiga picha na mwanaume mwingine wakati huku nyumbani amemwacha ‘mchumba’ ‘ake, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’.
CHANZO:GPL



No comments:
Post a Comment