ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 30, 2010

Ahadi za wagombea urais Muungano, Z`bar hizi hapa

Mwandishi wetu 
Baada ya hekaheka za kampeni kwa takribani miezi miwili na siku kadhaa, hatimaye Watanzania waliojiandikisha kupiga kura kuchagua diwani, mbunge na Rais watapata fursa hiyo ya kikatiba kesho.
Pamoja na ilani na sera za vyama vya siasa ambavyo vimesimamisha wagombea kuanzia ngazi ya urais, wagombea hao wametoa ahadi mbalimbali wakati walipokuwa wakinadi sera za vyama vyao.
Zifuatazo ni baadhi ya ahadi za wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar.

JAKAYA KIKWETE (CCM)
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la viwanda.
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria.
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (Shirecu).
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini.
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono.
7. Kuwapatia matrekta wakulima.
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi mkoani Kagera.
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi.
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba Mjini.
11. Kujenga uwanja wa ndege wa kisasa Kigoma.
12. Mutukula kupatiwa umeme kutoka Uganda.
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika Gridi ya Taifa ya umeme
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
15. Kuharakisha hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino.
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba.
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali.
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika.
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu.
20. Wilaya ya Geita kuwa na hadhi ya mkoa Januari mwakani.
21. Kulinda Muungano kwa nguvu zote.
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa.
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa.
24. Kujenga bandari ya Kasanga.
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo.
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira.
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama.
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini.
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es Salaam.
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same.
31. Kuboresha barabara za Igunga.
33. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu.
34. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya.
35. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipun guzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN).
36. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa.
37. Kulinda haki za walemavu.
38. Kujenga barabara ya Njombe kwa kiwango cha lami, urefu wa kilomita 109.
39. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha.
40. Kuanzisha jimbo la Bulyahulu, Shinyanga
41. Kujenga barabara ya lami kuanzia Manyoni-Kigoma hadi Kaliua.
42. Kukarabati barabara ya Arusha-Moshi.
43. Kuboresha barabara ya Handeni- Kondoa-hadi Singida.
44. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 huko Longido.
45. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga- Kahama kuunganishiwa maji.
46. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha.
47. Kukopesha wavuvi zana za kilimo.
48. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido, Loliondo.
49. Kujenga barabara ya lami kupitia pem bezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti.
50. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri.
51. Kusambaza maji nchi nzima.
52. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima, mwaka 2010-2015.
53. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha
54. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika.
55. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania.
56. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi.
57. Kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2015.
58. Kuwapa wanawake nafasi zaidi.
59. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii.
60. Kuipandisha hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa.
61. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada.
62. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay.
64. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 Mbambabay.
65. Kufufua chama Kikuu cha Ushirika Cha Wakulima wa Mbinga (Mbicu).
66. Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania.
68. Mtwara kuwa mji wa viwanda.
69. Ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuangamiza viluilui vya mbu.
70. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa.
71. Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalum la viwanda.
72. Kujenga machinga compex kila wilaya Dar es Salaam.
73. Wanawake kupatiwa chanjo ya saratani nchi nzima.
74. Ujenzi wa reli kutoka Ubungo hadi Tegeta, Dar es Salaam.
75. Tatizo la Maji Dar kuwa historia.
76. Kujenga chuo kikuu Shinyanga.
77. Kujenga chuo cha madaktari Ruvuma.
78. Kuboresha bei nzuri ya mazao.
79. Kujenga kiwanda cha kusindika mazao Kibaha.
80. Kufufua miundombinu ya reli kutoka Tanga kwenda Arusha.
81. Kutekeleza mradi wa umeme katika mto Rusumo mkoani utakaotoa umeme kwa mikoa ya Kagera, Kigoma.
DK. WILLIBROD SLAA (CHADEMA)
1. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa Rais.
2. Kukata asilimia 15 ya mishahara ya wabunge na kuongeza mishahara ya watumishi wa umma.
3. Kima cha chini cha mishahara ya
watumishi wa umma kuwa Sh. 350,000.
4. Kuunda Baraza la Mawaziri wasiozidi 20 pamoja na wasaidizi wao.
5. Kuuza ndege ya Rais na kununua helikopta ili kumwezesha kutua kila kijiji.
6. Elimu ya lazima kuanzia chekechea hadi kidato cha sita.
7. Kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha sita.
8. Kutoa huduma za afya bure.
9. Wananchi wanaozungukwa na migodi kuwa wanahisa ndani ya migodi.
10. Kufumua mikataba yote ya madini.
11. Kufuta misamaha ya kodi ya mafuta kwenye kampuni za madini.
12. Kushusha bei ya vifaa vya ujenzi kama saruji na bati kuuzwa chini ya Sh. 5,000.
13. Kutunga sheria itakayopiga marufuku ujenzi wa nyumba za nyasi ‘tembe’ hasa baada ya kushusha bei ya vifaa vyote muhimu.
14. Kujenga reli na treni mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa saa tatu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.
15. Kuunda Katiba mpya ndani ya siku 100.
16. Kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji ndani ya siku 100.
17. Kufuatilia Sh. bilioni moja zilizotolewa na serikali kwa kila mkoa ili kubaini na kuwachukulia hatua wajanja wachache walionufaika nazo.
18. Kuwarudishia wananchi mbegu zao walizokuwa wamepanda katika mfuko wa Development Entrepreneurship Community Initiative (Deci).
19. Kuwekea utaratibu utakaowawezesha wafugaji, wavuvi na wakulima kujiunga na bima.
20. Kuwachukulia hatua za kisheria wezi wote wa fedha za umma.
21. Kurudisha pesa za mradi wa rada.
22. Kujenga nchi isiyo na ufisadi.
23. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili Muungano wa Zanzibar.
24. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo.
25. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
26. Kutoa ruzuku taasisi za kidini
27. Kusambaza magari aina ya shangingi kwa Jeshi la Polisi ili wakamatie wahalifu, badala ya mawaziri kuyatumia
28. Kuimarisha uchumi, ajira na ujira bora na kutoa mafao kwa wazee
PROFESA IBRAHIM LIPUMBA (CUF)
1. Kubadili Katiba na kumteua Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais.
2. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi Chuo Kikuu.
3. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri.
4. Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
5. Kusimamia rasilimali.
6. Kuimarisha miundombinu.
7. Kusimamia na kuboresha sekta ya afya.
8. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji.
9. Kudhibiti uuzaji ovyo wa zao la korosho.
10. Kuanzisha mfuko maalum wa kusomesha walemavu.
11. Kushughulikia ufisadi.
MAALIM SEIF SHARIF HAMAD (CUF)
1. Kuigeuza Zanzibar kuwa kama Hong Kong.
2. Kuendeleza mashamba ya Karume.
3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya Zanzibar.
4. Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec)
5. Kuwaunganisha Wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano.
6. Kuwasilisha hoja ya kubadili Katiba ya Zanzibar na ya Muungano
7. Kuondoa bajeti ya Zec chini ya Waziri Kiongozi na badala yake kuwa inayojitegemea.
8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria
9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi
10. Kujenga jamii yenye maelewano na umoja.
11. Kutochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu.
12. Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi.
13. Kukomesha rushwa.
Kuhakikisha utoaji wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni.
15. Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh. 150,000.
16. Kubadili vikosi vyote vya usalama na kulipwa mishahara kima cha chini Sh.180,000.
17. Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao.
18. Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure.
19. Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita.
20. Kutoa kitambulisho cha Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi.
21. Kila Mzanzibari kupata pasi ya kusafiria.
22. Kuanzisha Shirika la Ndege Zanzibar.
23. Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka asilimia 6.8 hadi 15 kila mwaka.
24. Kutoa uhuru zaidi kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar.
25. Kuweka hadharani nambari yake ya simu.
26. Kubadili sheria ya uwekezaji.
28. Kutomhurumia Waziri au mkewe anapokosea ikithibitishwa kufungwa.
29. Kujenga bandari ya Mkokotoni na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi
30. Kudhibiti kuvuja kwa mitihani.
31. Kurejesha chakula bure kwa wagonjwa hospitali za serikali.
DK. ALI MOHAMMED SHEIN (CCM)
1. Kuboresha maisha ya wavuvi.
2. Kusomesha wafanyakazi.
3. Kipaumbele katika elimu.
4. Kipaumbele katika afya.
5. Kuulinda Muungano.
6. Kuleta mabadiliko Zanzibar.
7. Kuboresha Bandari ya Zanzibar kwa kuijenga upya.
8. Kuboresha Maendeleo Zanzibar.
9. Ujenzi wa maktaba kubwa na nzuri Kisiwani Pemba.
10. Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar.
11. Kuimarisha miundombinu Kisiwa cha Pemba.
12. Kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Pemba katika miradi mbalimbali.
13. Eneo la Micheweni kuwa maeneo huru ya uchumi.
14. Kumaliza matatizo ya maji mkoani.
15. Kujenga Bandari ya kisasa katika eneo la Mpiga Duri Unguja.
16. Kuiamrisha makazi bora kwa Wazanzibari.

No comments: