Kuna mpango wa bima unajadiliwa na NSSF utakaowezesha,Watanzania waishio nje kulipa kama $200 kwa mwaka,bina itakayowezesha wewe na ndugu zako Tanzania kufaidika nayo.
Bima hii itaruhusu NSSF kugharamia matibabu kwa ndugu yako Tanzania na kama itatokea Mwenyezi Mungu amekuchukua,NSSF itagharamia 100% kusafirisha mwili na msindikizaji mmoja.
Mpango huu upo mbioni na bado unajadiliwa,utakapokua tayari tutaleta taarifa zaidi.
1 comment:
Mbona pesa hizo ni nyingi sana! maana fuso zinarudi tupu kuelekea Iringa, Makambako, Songea na Mbeya. Wakipata msiba jamaa hufurahi kishezi, maana unawajazia mafuta ya 70,000 tu, mashine inacheua hadi inawafikisheni nyumbani kwenu. Hata watani zenu wa jadi ambao hungojea Fuso ya msiba ndipo warudi nyumbani huruhusiwa kupanda na sio mtu mmoja tu! Uzuri msiba unashushwa hadi mlangoni tena saa 10 hadi 11 asubuhi hapo ni Iringa, kabla jamaa hawajaanza kuitafuta Mafinga! Anyway, usumbufu wao wa kudai mafao umeisha? Maana hilo tu hawajaweza kulitatua, je hili amabalo ni nyeti wataweza?.
Post a Comment