Syllesaid Mziray 'SUPER COACH' (pichani kulia) ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam amefariki dunia leo alfajiri. Mziray, ambaye mpaka kifo chake alikuwa akimsaidia Kocha Phiri (pichani kushoto) kuinoa Timu ya Simba, alikuwa pia ni mwajiriwa wa Chuo Kikuu Huria kama Mhadhiri. Mipango ya mazishi na taarifa kamili zitawajia baadae. Tunatoa pole kwa wafiwa, jamaa na wanachama wote wa Klabu ya Simba kwa msiba huu. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi - amina!

...Marehemu Mziray akiwa kiwanjani akifuatilia mechi

..hapa akitoa moja ya mada zake katika masuala ya michezo hivi karibuni.
PICHA KWA HISANI YA GPL
No comments:
Post a Comment