
Vurugu zimetokea mapema leo katika kituo cha kupigia kura Mwananyamala, Kata ya Makumbusho baada ya mgombea nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya CCM, Bw. Christopher Mutayobwa kudaiwa kutoa bastola ili kujihami. Mgombea huyo imedaiwa alifikia hatua hiyo baada ya kuzongwa na wapiga kura waliomtuhumu kuleta mamluki kituoni hapo kwa ajili ya kumpigia kura, madai ambayo baadae yalikanushwa na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Elius Kalinga ambaye alisema tuhuma za kuleta mamluki hazikuwa za kweli na baadhi ya wnanachi waliosababisha vurugu hizo walitiwa mbaroni. Pichani ni Kamanda huyo akiongea na wanahabari kuhusu tukio hilo.
..wananchi wakiwa wamesimama pembeni baada ya jeshi la polisi kuwasili eneo hilo na kurejesha hali ya utulivu
...Kamanda Kalinga (kulia) akipewa maelezo ya vurugu hizo kutoka kwa afisa wake
...wananchi wa eneo la Mwananyamala wakiwa katika hali ya taharuki baada ya diwani huyo kutoa bastola.
PICHA: Richard Bukos/GPL



No comments:
Post a Comment