Ndugu wapendwa,
Sisi familia ya Salukele tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati, kwenu wote mlio jumuika katika kuwezesha kufanikisha kumsafirisha Marehemu baba yetu Mzee Mathew Salukele nyumbani Tanzania. Marehemu alizikwa siku ya Jumamosi tarehe 10/16/2010. Wakati tukiwa na mshangao,majonzi na uchungu mkubwa kwa kumpoteza baba yetu mpendwa kwa ghafla, Jumuiya ya watanzania hapa Columbus wameongoza shughuli zote za sala na michango ya hali na mali na tungependa kuwashukuru kwa moyo wote. Tungependa pia kutoa shukrani zetu za dhati kwa Jumuia za Watanzania kutoka nje ya Columbus na majirani zetu kutoka Kenya, Uganda na Zambia kwa misaada yao ya hali na mali.
Hakuna neno la kusema ambalo tunaweza kufananisha na upendo wenu usio na kikomo ambalo tutalinganisha na ukarimu wenu katika kipindi hiki kigumu. Wengi wenu mlisimamisha kazi zenu, masomo yenu, biashara zenu na shughuli zenu mbalimbali kwa ajili ya kutufariji. Uwepo wenu na maombi yenu yameweza kutufariji kwa kiasi kikubwa na kututoa ukiwa nakujiona kama familia moja. Tungependa tuendelee kushirikiana kwa moyo huu, na hii iwe changamoto kwa jumuia zote.
Jina la Bwana litukuzwe na Mungu awe nanyi daima.
Asanteni sana
Mungu awabariki
Familia ya Salukele.
No comments:
Post a Comment