Advertisements

Thursday, October 21, 2010

Stars kukipiga na Boston Rangers,Jumamosi,Uzinduzi VIJIMAMBO

Stars United
Boston Rangers
Timu ya Stars United itaingia dimbani kupepetana na Boston Rangers kutoka Massachusetts jumamosi October 23 kwa mechi kabambe itakayowakutanisha mahasimu wa jadi.

Mechi hii ni kama Yanga na Simba,ambapo mafahali hao wakutanapo ziumiazo ni Nyasi;
Timu ya Boston itaingia Jumamosi asubuhi wakiwa tayari kwa mpambano huo wa kukata na shoka utakaochezwa saa nane kamili kutokana na kuwapa nafasi wachezaji na mashabiki kuweza kujitayarisha ili kuwahi Bash la Uzinduzi wa VIJIMAMBO ambalo litaanza saa moja kamili usiku.

Mtanange unatarajiwa kuwa mkali kutokana na historia ya timu hizi mbili,mara ya mwisho timu hizi zilipokutana zilitoka 0-0 mechi iliyochezewa Cambridge,Massachusetts,ambapo mechi ya awali Stars walikula kibano 3-2 dhidi ya timu hii ya Boston,mechi iliyolalamikiwa na wachezaji wa Stars kuwa Refa aliibeba Boston Rangers.

Stars wanaichukulia mechi kua ngumu kutokana na uhodari wa wachezaji wa Boston na wengi wao wakiwa wameishachezea vilabu vikubwa kama vile Simba,Malindi na Small Simba na wengi wa wachezaji wao wakiwa wadhoefu wa ligi za madaraja ya chini.

Mgeni rasmi wa mpambano huu atakua Paul Rwechungura aliyekua Golikipa mahili wa TP LINDANDA(Pamba ya Mwanza)

mechi itachezewa NEW CARROLLTON YOUTH MEMORIAL PARK  (New Carrollton) 7500 Good Luck Road, New Carrollton, Md. Beltway I-95/495 to Exit #23, Kenilworth Avenue, toward Bladensburg, left on Good Luck road, field is on your left across from Robert Frost Elementary School. P.9.k.3
Karibuni mashabiki usisahau mechi ni saa nane kamili

No comments: