MAHAKAMA ya wilaya ya Maswa imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu mkazi wa kata ya Ipililo wilaya Maswa kwa hatia ya kupiga kura mara mbili katika uchaguzi mkuu jana.
Hakimu Thomas Mtani amesema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya utetezi wa mshtakiwa huyo na kumkuta na hatia anastahili adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Kutokana na utetezi kuwa hajawahi kushtakiwa na pia mahakama kumuona kuwa ni mtu mzima anayetambua kuwa ni kosa kupiga kura mara mbili, mahakama imeamua kumpa adhabu bila faini ili iwe fundisho asirudie tena.
No comments:
Post a Comment