
gari la Chenge lilohusika katika ajali hiyo
Bajaji iliyogongwa na kuua abiria wawili waliokuwemo, ambapo dereva alipona na hakupatikana hadi leo.
Na Iddi Sandaly
Thamani ya Binadamu haiwezi kulipwa kwa pesa wala mali ya aina yeyote. Vifo hivi vimesababishwa na Muheshimiwa Chenge kwa kuendsha bila kuwa makini vimeadhiri kiasi kikubwa sana mpaka kuletea mdogo wake Mareheme mmoja kujinyonga.http://www.thecitizen.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/6794-chenge-road-accident-victims-family-speaks-out.html .
Sasa ikiwa kama muheshimiwa Chenge amekutwa na Makosa ya kuwa amesababisha vifo, naona ingebidi atozwe faini ambayo inaleta maana na sio kumwambia ati alipe shillingi 700,000, ambayo ni sawa na dola za kimarekani 479. Kumbuka ni huyu huyu Chenge aliye ishitaki NBC ili alipwe Shilingi Milioni Mia tatu na kumi (310,000,000), sawa na dola za kimarekani 212,183, kwa sababu ati walitowa habari zake za kifedha bila ruhusa yake.http://www.thecitizen.co.tz/news/4-national-news/1514-chenge-sues-nbc-for-sh310m.html . Yeye anatozwa faini ya laki saba kwa kuuwa watu wawili.
Huu ni mzaha wa kutokuthamini Maisha ya watu na ni masihara makubwa sana na inabidi swala hili likemewe kwani haiwezekani kumuhukumu mtu miaka mitatu au faini ya hali ya chini kama hii; Maswali ambayo tukiwa sisi ni watahiniwa ambao pia tunaweza siku moja kukumbwa kwenye ajali kama hizi. Je Shilingi laki saba ni faini au Masihara; Je insurance coverage ina nafasi gani kwa watu wanaopatwa na ajali na kupoteza maisha yao au kupata vilema vya kudumu.
Ni lazima tujaribu kuwa wenye kuleta maana kwa hukumu zetu na maamuzi yetu; huu ni mfano mmoja tu ambao muheshimiwa Chenge kasababisha maafa lakini kuna maisha ya watu wengi sana yamepotea au kuharibiwa kwa kupewa ulemavu wa kudumu kutokana na uzembe wa madereva wetu .
Nilazima kila mtu awajibike kuanzia Mashirika ya bima na serikali. Inabidi serikali iimarishe sheria za uendeshaji na utowaji wa leseni. Mashirika ya Bima yakishirikiana na serikali inabidi yaweke viwango vya juu vya bima. Ikiwa ni pamoja na Malipo bora kwa watakao umia au kupoteza Maisha.
No comments:
Post a Comment