Baadhi ya ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu muda mfupi baada ya mwili kuwasili Kijijini Kibanda.
Mazishi ya aliyekuwa mwanamuziki na Meneja wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ Abou Semhando ‘Baba Diana’ yalifanyika saa 9:00 Adhuhuri Desemba 19 mwaka huu katika Kijjiji cha Kibanda, Muheza Tanga.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa kijiji hicho pamoja na majirani pamoja na baadhi ya wanamuziki wa bendi mbalimbali kutoka jijini Dar es Salaam.
Aidha, mazishi hayo yalihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mhe. Idd Azzan.
Mmoja wa waombolezaji akiagua kilio baada ya kuona mwili wa marehemu.
Kiongozi wa Bendi hiyo Luiza Mbutu akilia kwa machungu.
Mkurugenzi wa Bendi hiyo Asha Baraka alijumika katika sala ya kuuombea mwili wa marehem muda mfupi kabla ya mazishi.
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho na wanamuziki wa Twanga wakiwa wamebeba mwili tayari kwa mazishi.
Mbuge wa Kinondoni, Idd Azzan akielezea jinsi alivyokuwa akimfahamu marehemu muda mfupi kabla ya mazishi.
Picha: Brighton Masalu/GPL
No comments:
Post a Comment