Bendi maarufu nchini Tanzania, African Stars 'Twanga Pepeta', imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na kiongozi na mwanamuziki wake mkongwe, Abuu Semhando 'baba diana' aliyefariki dunia alfajiri ya leo baada ya kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki. Habari zaidi zinasema kuwa marehemu aligongwa na gari aina ya Mercides Benz wakati akitoka kwenye onesho la muziki lililofanyika Aficana, maeneo ya Mbezi jijini Dar es salaam. Mara baada ya kugongwa na gari hilo, ambalo lilisimama, marehemu angeweza kupona, lakini alikanywagwa na magari mengine yaliyokuwa yakitokea Mwenge. (Pichani juu ni baadhi ya wanamuziki wa twanga, akiwemo Aisha Madinda wakilia kwa uchungu katika hospitali ya muhimbili)
Mkurugenzi wa African Stars, asha Baraka, akiwa katika taharuki kubwa hospitalini mara baada ya kifo cha mwanamuziki wake, ambaye alikuwa ni mpiga drum maharini na ambaye kabala ya kuondoka, alipiga drum kwa mara ya mwisho katika wimbo wa Mwanadaraesalama.
Maimatha akiwasili muhimbili akiwa pekupeku.
Pichani ni marehemu Abuu Semhando. Picha hii alipigwa katika viwanja vya Biafra wakati wa kumuaga marehemu Dk.Remmy , aliyegwa katika vianja hivyo Alhamis Desemba 16 jijini Dar.
PICHA: ISSA MNALLY NA SHAKOOR JONGO/GPL
No comments:
Post a Comment