ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 31, 2010

SUMU 10 ZINAZOWEZA KUKUWEKA NJIAPANDA KATIKA MAPENZI



Daima Mungu ataendelea kuwa juu ya kila kitu kwenye Sayari ya Dunia na nyingine zote, kwani yeye ndiye muweza wa yote. Utukufu wake ndiyo unaotupa fursa tulizonazo, tunaishi kulingana na matakwa yake, kwahiyo sisi siyo lolote mbele yake.
Tumshukuru na kumhimidi kwa kila hali, wakati huo huo, nakukaribisha katika uga wako uliochanja mbuga wa XXLOVE. Hii ndiyo safu yako pendwa ambayo inakupa gerentii ya kusoma na kuelimika kuhusiana na mambo ya mapenzi.

Tunazungumzia mapenzi katika sura ya kipekee kwakuwa yanahitaji thamani ya hali ya juu. Yanaheshimiwa kupita kiasi kwa sababu yenyewe ni sanaa kiranja ambayo kila mtu lazima atayapitia. Tunapenda na kupendwa, hivyo tupo mapenzini! Ambaye hayumo, basi pengine mambo yake siyo mazuri!
Hata hivyo, binadamu hatuko sawa, kila mtu anayo tafsiri yake anayoijua kuhusiana na mapenzi, ndiyo maana hatuachi kuelekezana. Naandika kwa kushauri na kukosoa kwa sababu huu ndiyo wajibu wangu katika safu hii.
Kila mmoja anapoingia katika uhusiano wa kimapenzi, moja kwa moja ndoto zake huwa ni kumfanya mwenzi wake kuwa wa kudumu. Atajiwekea malengo hata yasiyotekelezeka ilimradi airidhishe nafsi yake.

Hujawahi kuona mtu anapata mwenzi leo, kisha akaanza kupiga mahesabu ya kufunga naye ndoa? Ukweli ni kwamba wengi wetu tunapopata penzi jipya, tunakuwa na matarajio mengi. Ni vizuri kuwa na matarajio na kujiwekea malengo ya kuyatimiza, lakini kosa kubwa ni kwamba huwa tunajisahau katikati ya safari.
Tunapenda kudumu na wenzi wetu tunaowapata, lakini ndoto hizo hugeuka za alinacha kama si kitendawili kwakuwa hatuwezi kujirekebisha ama kuficha makucha. Matunda ya hali hiyo ni kuwa na kizazi chenye kujiwekea matarajio ya mashaka kila siku.

Pointi ya msingi hapa kama kweli tunataka kuwa na mapenzi ya kudumu ni kujua udhaifu wetu angali bado mapema. Kutambua mambo ambayo ni sumu, zinazoweza kuuua uhusiano wetu ili tuzichukue kama changamoto, kisha tuzikabili na kushinda.
Hapa chini, nimekuandalia tabia 10 ambazo ni sumu katika mapenzi. Hizi, zinaweza kuubomoa uhusiano wako ndani ya muda mfupi. Muhimu ni kuzijua ili utambue namna ya kuziepuka.

UVIVU
Hii ni sumu kali, lakini ni rahisi kuiepuka kama utaamua. Asili ya umbile la kila binadamu, ndani yake kuna uvivu. Na ni vizuri kutambua kuwa katika vitu ambavyo ni rahisi kumchefua mwenzi wako ni hili la uvivu.
Uvivu unaweza kuwa wa kujishughulisha katika mambo ya nyumbani ama wa utafutaji wa riziki. Lakini baki ukijua kwamba tabia hiyo inakufanya ukalie kuti kavu kwenye uhusiano wako.
Unashindwa kumsaidia mpenzi wako kazi ndogo ndogo, unangaalia nguo chafu haujitumi kuzifua, nyumba haitamaniki, hujiwezi kwa lolote, tabia yako hiyo, inampa mwenzio tiketi ya kukuacha.

Pointi hii, inastahili kupigiwa mstari mwekundu kwa wanawake. Ni rahisi mwanaume kuvumilia kasoro chache alizonazo mwenzake, lakini siyo ya namna hii. Muhimu ni kutambua ya kwamba uvivu utakupunguzia heshima na mvuto wako katika mapenzi.
Aidha, kwa mwanamke ni janga ambalo mwanaume hatokawia kulikimbia. Unadhani atawezaje kuvumilia kuwa na mtu ambaye hajiwezi kwa lolote? Kujishughulisha hutaki, kuwajibika katika uwanja wa kuta nne ni tatizo! Atajiuliza: Ni faida gani ya kuwa na wewe?
Achana na uvivu wa kazi za kila siku, pia unapaswa kuwa mwepesi linapokuja suala la kushughulika kimapenzi. Namaanisha uwanjani!

UCHAFU
Tabia hii, inaenda sambamba na uvivu. Kwa kifupi ni kwamba uchafu ni matokeo ya uvivu. Mtu asiyejiweza kwa lolote hatomudu usafi, hivyo kutia sumu kwenye uhusiano wake.
Una tabia ya uvivu, kwahiyo ni mchafu, unapaswa kutambua kuwa mwenzi wako anakerwa mno na tabia yako. Anza kwa kujichunguza mwenyewe ili kujua wewe ni mchafu kwa kiwango gani. Jawabu lako, linaweza kukusaidia kwa kiasi cha kutosha, ikiwa utaamua kubadilika.

Unavaa nguo mpaka zinatoa harufu mbaya, ukiongea, unatoa hewa chafu ya mdomo, kuoga kwa wasiwasi hadi mwili unanata, unashindwa kudhibiti jasho lako, mpaka unawasumbua wenzako kwa sababu ya kikwapa. Kwa hali hiyo unategemea nini?
Tuweke kituo kikubwa kwa leo, panapo majaliwa tukutane Jumatatu, tupate kuendelea na mada yetu hii. Ushirikiano wako bado nauhitaji, kwahiyo tumia namba yangu hapo juu kwa ushauri au maoni.
Tukutane Jumatatu

Askofu wa Ireland ajiuzulu Nigeria


Nigeria
Makao makuu ya kanisa la Kikatoliki Vatican imekubali hatua ya kujiuzulu kwa askofu wa Ireland aliyekuwa Nigeria kutokana na shutuma za kumdhalilisha kijinsia binti mmoja huko Niger Delta.
Richard Burke, askofu wa mji wa Benin, amekubali kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti huyo lakini amekana kwa binti huyo kuwa na umri mdogo uhusiano huo ulipoanza.
Katika taarifa iliyotolewa kwenye gazeti la kikatoliki la Ireland amesema, " Sababu ya kujiuzulu ni kutokuwa mwaminifu katika kiapo changu cha useja."
Askofu huyo amejiuzulu baada ya madai hayo kutolewa mwaka jana.
Dolores Atwood alidai kunyanyaswa kijinsia na askofu Burke wakati alipokuwa padri huko Warri kusini mwa Nigera kwenye mji wa Niger Delta.
Hata hivyo, amesema uhusiano wao ulianza mwaka 1989 alipokuwa miaka 40 na binti akiwa na umri wa miaka 21.
Amesema kwenye taarifa yake, " Nilijibu haraka iwezekanavyo kwamba sijawahi hata siku moja maishani mwangu kumnyanyasa mtoto kijinsia. Huu bado ni msimamo wangu. Huu ni ukweli."
Askofu Burke pia alimwomba radhi Bi Atwood na kuomba msamaha katika vituo vyake vya kanisa huko Warri na Benin.
Kanisa hilo limesema limekubali kujiuzulu kwake ambapo pia limetaja jopo litakalochunguza udhalilishaji wa watoto
uliofanywa na viongozi wa kikatoliki huko Ireland.

Menyu ya ughaibuni,hapa vimekosekana vitumbua!!!!!!!!

MISS SINZA 2010

SIREFA yamfagilia Mo Dewji,kupongezwa kwa tafrija fupi Regency hotel


Na Andrew Chale
Uongoazi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Singida (SIREFA) umemmwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini na Mjumbe wa NEC-CCM Mkoa,  Mohammed Gulam Dewji kwa changamoto za kuinua soka mpaka timu hiyo kutwaa kombe la Taifa maarufu kama Kill Taifa Cup.
Akiongea na blog hii leo mchana kwa njia ya simu Katibu wa Chama cha Soka Mkoa huo, Hussein Mwamba alisema alishukuru uwongozi mzima wa mkoa huo kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na wao kunyakuwa ubingwa huo.
Mwamba alisema kuwa wanakila sababu ya wao kumshukuru Mo Dewji kwa kutia amasa katika maswala ya michezo.
“Mo Dewji ameweza kuimalisha mambo mbalimbali ya kimichezo ndani ya mkoa wa Singida, hivyo tunakil sababu ya kujivunia kwa ubingwa huu ambao umechangiwa kwa amasa zake” alisema Mwamba.
Pia Mwamba alisema kombaini ya timu hiyo ya mkoa wa singida karibu nusu nzima wanashiriki kombe la Mbunge huyo maarufu kama ‘Mo Cup’ ambapo ushindaniwa kila mwaka jimboni humo.
“Tukiwa kama viongozi tunawapongeza wote waliofanikisha ushindi mpaka kutwa ubingwa huu ambao tunaahidi tutautetea kila mashindano haya” alisema.
Kwa upande wake, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi iwa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL)   ambaye  yupo nje ya nchi, Ufaransa, akiongea kwa njia ya simu aliipongeza timu hiyo na kuwataka kuendeleza moyo huo huo.
“Nimefurahi sana kwa matokeo ya kunyakua ubingwa na kuiwakilisha vyema bendera ya MKOA WA Singida, hii iwe ni miaka yote na kuifanya Singida ionekanae inapaaa” alisema Mo Dweji.
Singida Yetu inapaa hivyo tunakila sababu ya kujjivunia uashindi huo wa mkoa mzima.
Mo Dewji aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni tano kwa timu hiyo pindi itakapotwaa ubingwa, hivyoo kwa matokeo hayo timu hiyo imeweza kutimiza ahadi.
Kufuatia Mo Dewji kuwa nje ya nchi, fedha hizo zinatalajiwa kutolewa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya MeTL kwa niaba ya Mo Dewji.
“Tunapanga alfa maalum kwa ajili ya kuwakabidhi fedha hizo ambapo watakabidhiwa na Mwenyekiti wa MeTL, Gulam Dewji, ambaye ni baba mzazi wa Mo, alisema Afisa uhusino na msaidi wa Mbunge huyo.
Timu ya Mkoa wa Sinngida ‘Kindai Shooting’ mwishoni mwa wiki ilifanikiwa kutwaa kombe hilo  kwa mara ya kwanza kwa kuwafunga timu ya Lindi 3-0, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar e Salaam.
Mbali na pongezi hizo, Mwamba aliwataka wanasingida kuendelwea kuusaidia mkoa huo ili uendelee kukuwa katika soka kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. “Miaka mitano iliyopita tulikuwa na timu iliyoshiriki ligi kuu bara, hivyo matarajio yetu sasa ni kuona tunapata timu ya kuwakilisha ligi kuu” alisema.
Aidha, Mwamba alisema timu hiyo  leo jioni watakuwa na tafrija fupi ya kupongezana huku viongozi wote wa mkoa wa Singida watajumuika pamoja.
“hee mpaka sasa bado ni furaha tu, leo kuanzia saa 2;00 usiku tutakuwa katika Hotel ya Regence Park Hotel kwa kupongezana na kisha tunatarajia kuondoka alfajiri ya Jumatano na kuendeleza shangwe huko Singida” alisema Mwamba.


Image
Rais wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume akizungumza na Waziri wa Habari na Vijana wa Qatar, Abdulaziz Bin Hamad Gaway mara baada ya kuwasili katika uwaja wa ndege wa Kimataifa wa Doha, mjini Qatar ambako anahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi (WEF), (Picha na Abadalla Haji, Doha)

Sunday, May 30, 2010

Wakazi wa Magomeni; Walalamikia Bonde la Mkwajuni,Magomeni


Na Andrew Chale


WAKAZI wa Magomeni na Mkwajuni Manispaa ya Kinondoni wamelitaka jeshi la Polisi kuimalisha Ulinzi katika bonde la Mkwajuni,kufuatia vibaka kupola na kujeruhi wananchi nyakati za usiku.
Wakizungunza na.......... jana kwa nyakati tofauti jana jijini Dar esa Salaam wakazi hao, walidai kuwa  wanakabiliwa na wakati mgumu kutoka kwa vijana wa kihuni ambao wanakaba wapiti njia majira ya jioni na kuwanyang’anya mali pamoja na kujeruhi.
Mengi ya madai hayo wakazi hao walidai kuwa Diwani wa Kata ya Magomeni Julian Bujugo   alidai kuwa ameshindwa kuondoa kero za wanchi ambao wanakabiliwa na usalama mdogo.
“Diwani wa Kata ya Magomeni, ameshindwa kutatua tatizo ili kwa muda mrefu sasa, msitu huu umekuwa ukipoteza maisha ya watu na mali zao kila siku lakini yeye ameshindwa kuingilia kati’ walisema wakazi hao walipokuwa wakionghea na........
Wakazi hao waliendelea kudai kuwa, licha ya kulipoti kero zao hizo, katika vyombo vya usalama lakini hamna hata maamuzi sahihi yaliyochukuliwa huku kil siku wakishambuliwa na vibaka wanao jificha kwenye poli hilo.
“Tumelallamika juu ya swala ili kwa muda mrefu sasa juu ya kuondolewa huu msitu, upunguzwe ama utolewe kabisa lakini hamna hatua zilizochukuliwa” walidai.
Uchunguzi uliofanywa na ...... ili kwa siku kadhaa, uliweza kubaini matukio mbalimbali ya kihalifu wanaofanyiwa wapitanjia, yakiwemo ya kupolwa mali mali zao na kudhuriwa.
Huku idadi kubwa ya wanaopolwa katika bonde hilo ni wapanda baiskeri wanaokatisha majira ya alfajiri ya asubuhi na jioni, ambapo wahalifu hao inadaiwa wanakaa katika poli hilo na pindi wanapofanywa uhalifu huo wanakimbilia humo.
“Wapanda baiskeri mara kwa mara wanapolwa, tunaomba wasiwe wanajiamini kukatisha katika bonde hili majira ya jioni ni hatari kwao pamoja na wapita njia” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo alipotafutwa Diwani wa Kata hiyo ,Bujugo akuweza kupatikana kulizungumzia swala hilo.

MSAKO WA PIKIPIKI MORO


Na Dunstan Shekidele,Morogoro,
KUTOKANA ogezeko la ajali za pikipiki kutokea kila mara Mkoani Mrogoro jeshi la polisi mkoani hapa limeendesha msako mkali na kukamata waendesha pikipiki hizo bila kuwa na leseni.

Mwandishi wetu alifika katika kituo kikuu cha usalama barabarani mkoa wa morogoro na kukuta lundo la pikipiki zikiwa zimekamatwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kosala la kuendesha bila leseni.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa morogoro[RTO] lbrahim Mwamakula alipohojiwa na mwandishi wetu kuhusiana na opresheni hiyo,alisema kwamba zoezi hilo limeanza juzi na kwamba zaidi ya pikipiki 82 zimekamatwa kwa makosa mbali mbali.

"Safari hii hatuta kuwa na huruma na mtu, juzi na jana tumeshakamata pikipiki zaidi ya 82 unazoziona hapo nje,na kwamba leo tumefanikiwa kuwapeleka mahakamni madereva 8 kwa kosa la kuendesha pikipiki bila ya kuwa na leseni na hawa ndio wanaosababsiha ajali nyingi,. alisema

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya morogoro,Bw Thabiti Said Mwambugu ameitisha semina ya madereva wote wa pikipiki wa wilaya ya morogoro mjini ndani ya ukumbi wa Bwalo la umwema

ANTI LULU ADATISHA!



Kimwana Manywele 2002 na, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni cha C2C, Lulu Semagongo aka Ant Lulu, akiserebuka na mnenguaji wa bendi hiyo Chipsi-Kuku. .
Kimwana Manywele 2002 na, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni cha C2C, Lulu Semagongo aka Ant Lulu, akimbinjukia Rapa wa akudo, Totoo Ze Bingwa wakati wa onesho la akudo jana Mango Garden .
Kimwana Manywele 2002, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni cha C2C, Lulu Semagongo aka Ant Lulu akimbinjukia paparazzi wakati anakata nyonga katika onesho hilo.
Wakazi wa jiji la Dar wakibanjuka katika onesho la Akudo Impact lililofanyika ukumbi wa Mango Garden usiku wa kuamkia jana

Wanaume wapendanao waachiwa Malawi

Wapenzi wa jinsia moja
Wanaume wawili wanaofanya mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi waliofungwa baada ya kufanya sherehe ya uchumba wamesamehewa na Rais Bingu Wa Mutharika.
Bw Mutharika, akizungumza wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alipotembelea nchi yake, amesema ameamuru waachiliwe huru haraka iwezekanavyo.
Steven Monjeza na Tiwonge Chimbalanga walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela mapema mwezi huu kwa kufanya vitendo kinyume cha maumbile na vitendo vya aibu.
Kesi hiyo iliibua malalamiko kutoka nchi za kimataifa napia mjadala juu ya mapenzi ya jinsia moja ndani ya Malawi.
Bw Ban ameusifu uamuzi wa Rais kuwa ni wa "kijasiri."
Amesema, "Sheria hii iliyopitwa na wakati irekebishwe popote ilipo."

'Utamaduni wa chuki'

Waandishi wanasema Malawi ni jamii yenye msimamo mkali sana ambapo viongozi wa dini huhusisha mapenzi ya jinsia moja na ushetani.
Bw Mutharika amewaachia huru kwa misingi ya haki za binadamu.
Baada ya kukutana na Bw Ban alisema, "Wanaume hawa wawili wametenda uhalifu dhidi ya mila zetu, dini zetu na sheria zetu."
"Hata hivyo, kama mkuu wa nchi nawasamehe na hivyo waachiwe haraka iwezekanavyo bila masharti yeyote."
Steven Monjeza, 26, na Tiwonge Chimbalanga, 20, walikuwa gerezani tangu walipokamatwa Desemba 2009 baada ya kufanya sherehe ya uchumba, kabla ya mipango ya kufunga ndoa mwaka 2010.
Gift Trapence, kutoka kituo cha kutetea maendeleo ya watu, amefurahiswa na uamuzi huo.
Amesema, "Tumefurahi sana na tunamsifu Rais kwa ukomavu wake, lakini bado tuna safari ndefu kumaliza mila hizi za chuki."

Sheria za kikoloni

Mashirika ya kutoa misaada na haki za binadamu yamekuwa yakishinikiza serikali yake kuheshimu haki ya wachache.
Wanaume hawa wawili wametenda uhalifu dhidi ya mila zetu, dini zetu na sheria zetu.
Bingu Wa Mutharika, Rais wa Malawi
Serikali ya Uingereza, mfadhili mkuu wa Malawi, ilisema ilishtushwa na hukumu hiyo, na Marekani iliuelezea kama hatua moja nyuma katika harakati za kupigania haki za binadamu.
Siku ya Jumamosi, mwanamuziki wa miondoko ya Pop Sir Elton John aliandika barua ya wazi kwa Bw Mutharika kupitia gazeti la Uingereza la The Guardian akiomba waachiwe huru.
Wanaume hao wawili wamehukumiwa kwa sheria ya zamani ya kikoloni wakati Malawi ilipokuwa ikitawaliwa na Uingereza.
Makoloni mengi yaliyokuwa ya Uingereza yana sheria sawa na hiyo inayopinga mapenzi ya jinsia moja: India ilibadilisha sheria hiyo ya kuwapinga mwaka jana.

Viongozi wa Asia wakutana Korea Kusin


Viongozi wa Asia nchini Korea ya Kusini
Viongozi wa Uchina, Japan na Korea ya Kusini wamekubaliana kufanya kazi pamoja katika kusuluhisha mzozo juu ya kuzama kwa manuari ya kijeshi ya Korea ya Kusini.
Baada ya kumalizika kwa mkutano wao nchini Korea ya Kusini, viongozi wa mataifa hayo wamefanya mkutano na waandishi wa habari.
Viongozi wote watatu walikubaliana kuwa kuzama kwa manuari ya Korea ya Kusini, ambapo watu 46 walipoteza maisha yao mwezi March, ni changamoto kubwa kwa usalama na utulivu wa eneo hilo.
Waziri Mkuu wa Japan,Yukio Hatoyama, ameahidi kumuunga mkono Rais wa Korea ya Kusini, Lee Myung-bak na ameongeza kuwa anakubaliana kikamilifu na ushahidi kuwa manuari hiyo ilililipuliwa na kombora la torpedo lililofyatuliwa na nyambizi ya Korea ya Kaskazini.
Msimamo wa Uchina baado haujabainika wazi. Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa Uchina, Wen Jiabao, alituma salamu za rambi rambi kwa familia za mabaharia waliouwawa, na akazungumzia umuhimu wa kutuliza hali ya wasiwasi iliyopo, lakini hakusema chochote kuhusu msimamo wake juu ya suala la Korea ya Kaskazini kuhusishwa na shambulizi hilo.
Utawala wa Beijing unadhaniwa kuhofia kumchokoza mshirika wake wa siku nyingi katika vita baridi duniani, huku Pyongyang ikikanusha vikali madai ya kuhusika na shambulizi la kombora dhidi ya manuari ya jirani wake, Korea ya Kusini

Habari Njema Kwa Wakazi Wa DMV

Wawili wafa Dar


na Andrew Chale
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la fundi kubanwa na mashine ya kuchang’anyia cement na mwinge kuzama maji katika ufukwe wa bahari ya Hindi.
Katika tikio la fundi ambaye aliyefahamika kwa jina la Mbaraka Mkongame(22) amefariki dunia baada ya kulaluliwa na mashine ya kuchanganyia Cementi.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema kuwa tukio ilo lilitokea juzi majira ya saa moja jioni  huko eneo la UFI, Urafiki.
Kalinga alisema marehemu alikumbwa na mauti hayo alipokuwa anachanganya cementi katika mashine hiyo na kuingiza katika bomba, ghafla mkanda wa Ovaroli aliyovaa ilinasa katika mashine hiyo na kumchana utumbo.
“Mashine hiyo ilimchana utumbo na kumlalua hadi utumbo kutoka nje sehemu za kitovu na kupelekea kifo chake hicho” alisema Kalinga.
Hata hivyo baada ya kutokea tukio hilo, walizima mashine hiyo lakini alikuwa tayari ameshapoteza maisha.
Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na uchunguzi unaendelea.
Katika tukio jingine,Kamanda Kalinga alidai kuwa mtu aliyefahamika kwa jina la Idd Salum (20) alifariki dunia alipokuwa akiogelea katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Jangwani Beach.
Kalinga alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12 jioni, ambapo inadaiwa marehemu alikutwa na mauti hayo baada ya kunywa maji mengi.
Mwili uliopolewa na wananchi waliokuwa jirani na ufukwe huo na kuifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha, Katika tukio jingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Msime  alisema kuwa huko katik barabara ya Nyerere banda la Ngozi  gari lililokuwa na namba T 2119 BCH aina ya Benz likiendeshwa na Naila Kalembo, ghafla liliteketea kwa moto na kuunguza gari lote pamoja na mali zilizokuwemo humo.
Kamanda Msime alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Kamata na kuelekea TAZARA, huku chanzo cha ajali hiyo na thamani nzima bado haijafahamika na uchunguzi unaendelea.

Kapitali wala bata na Hasheem Thabeet,Meadowbrook pk,MD


















Saturday, May 29, 2010

Memorial Weekend,Columbus Ohio From May 28-31 2010



Kundi Maarufu La KRYSTAAL kutoka Canada Litakuwepo


HOTEL & ACCOMMODATION
Concourse Hotel & Conference Center
4300 International Gateway
Columbus,OH,43219


SERVICES/HUDUMA
-Mafundisho ya neno la Mungu
-Huduma ya maombezi
-Kipindi cha maswala na majibu


MASWALI
Unafamilia? no problem
-Huduma ya watoto(DAY CARE)itakuwepo
-Under 18 ni FREE ADMISSION


HOTEL & ACCOMMODATION
-Single $40/= 
-Couples $60/=


For Additional Information Contact the Hotline
-(614) 218 0716
-(614) 622 0667
         OR
Bofya Hapa