ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 17, 2011

CHEKA UNENEPE

MUARABU ALISHITAKIWA KWA KOSA LA KUNYWA GONGO


na Uwesu Yusuff


Muarabu alishtakiwa kwa kosa la kunywa gongo yeye na
Mhindi yule Mhindi akakubali kosa akaachiwa mwarabu yeye akajibu "siku yote
fombe kharaam habana fombe halaal sasa takunywa namna gani kharaam?" 

hakimu akamwambia askari mpe kofi huyo. Askari hakuelewa kama anatakiwa ampe Mwarabu gahawa badala yake akamuasha kofi mpaka 
chini... Mwarabu alipoinuka.. nae akamshindilia askari ngumi mpaka chini... hakimu
akamuuliza "we kwanini unampiga askari?" mwarabu akajibu "yeye manipa Gahawa
mimi maruidisha kikombe yake!"


No comments: