ANGALIA LIVE NEWS
Thursday, January 6, 2011
Dk Wilbrod Slaa, Freeman Mbowe na Philemon Ndesamburo Wakiwa Kizimbani
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Mh.Wilbroad Slaa(kushoto)Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe(Kulia),na wabunge wa Moshi Mjini Mh.Philemon Ndesamburo na Goodluck Mrema(Hayupo Pichani)wakiwa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Leo,Viongozi Hawa Wakuu wa Chadema wamefikishwa mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomewa mashtaka kadhaa,likiwemo pamoja na kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano hapo jana lakini waliachiwa kwa dhamana leo
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa(mbele)na Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema wakiwasalimia wafuasi wa chama hicho mara baada ya kuachiwa leo mchana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakati kesi yao ilipokuwa ikisikilizwa.
Mamia ya wafuasi wa CHADEMA mkoani Arusha wakiwazonga askari polisi kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao ambao walikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwenye Mahaka ya Hakimu Mkazi Arusha Leo.Picha na Mdau Marc Nkwame na Msimbe Beda
Picha kwa hisani ya Hakingowi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment