ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 17, 2011

MKUTANO WA WATANZANIA,DMV

Watanzania wenzangu DMV najua wengi wetu tumejiandikisha kwa ajili ya mkutano na Mh.Balozi hapo January 29,2011 na kama bado basi zingatia siku zilizobaki ni chache,usisite kufanya hivyo kwani mkutano huu ni muhimu sana kwetu Watanzania tuishio DMV

Madhumuni ya mkutano huo yatakuwa yafuatayo:- 

(i)  Balozi kujitambulisha rasmi kwa Watanzania washio katika eneo la Washington DC Metro.
(ii)  Kuchagua na kuunda kamati ya muda itakayoandaa katiba mpya ya jumuiya na hatimaye kuitisha na kusimamia uchaguzi mkuu wa Jumuiya mpya ya watanzania waishio Washington DC Metro.
(iii)  Masuala mengineyo muhimu yatakayojitokeza yanayohusu watanzania waishio hapa Washington DC Metro.



MAHALI:
Hollywood Ballroom - 2126 Industrial Pkwy, Silver Spring-MD 20906 
(Sehemu ya maegesho ipo yakutosha)

MUDA:
Saa 10.30 jioni (Tafadhali zingatia muda)


Ili kukamilisha maandalizi ya mkutano huo, unaombwa kujiandikisha Ubalozini kwakuandika jina lako hapa chini.Sehemu hii ni salama(secure)nataarifa zako zitalindwa.
Maelezo yako ni kwa lengo la kufanikisha mkutano huo nakujenga takwimu kuhusu Diaspora ya Watanzania. Taarifa zote zitahifadhiwa kwa siri. 



Kwa kujiandikisha Bofya Hapa

No comments: