ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 6, 2011

Rais Jakaya Kikwete Audhuria Mazishi ya Waziri Mstaafu wa SMZ Salum Jum Othman Unguja

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiomba dua pamoja na Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein(wapili kushoto),Makamu wa kwanza wa Rais wa SMZ Seif Shariff Hamad(kushoto) pamoja na makamu wa pili wa Rasi wa SMZ Balozi Seif Iddi(kulia) wakati wa Mazishi ya Waziri mstaafu wa SMZ marehemu Salum Juma Othman yaliyofanyika huko Unguja leo mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kawenye kaburi la aliyekuwa Waziri mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Marehemu Salum Juma Othman wakati wa mazishi yake yaliyofanika huko Unguja leo mchana. Marehemu Salum Othman aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama na Serikali zikiwemo uwaziri,ukuu wa mkoa, katibu mkuu wa UVCC na mjumbe katika tume za jaji Warioba,jaji Kisanga na jaji Nyalali.Pembeni ni Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ Seif Shariff Hamad.Picha na Freddy Maro/ikulu

No comments: