ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 18, 2011

UONDOAJI WA SUMU MWILINI

Uondoaji wa sumu mwilini ni nini? Bila shaka unaweza kujiuliza swali hilo. Uondoaji wa sumu mwilini ni mchakato wa kuondoa sumu kutoka mwilini kwa njia mbalimbali.

Awali ya yote fahamu jambo hili. Kuna aina mbili za sumu ambazo hurundikana mwilini katika kipindi fulani. Kuna sumu zitokanazo na uchafuzi wa mazingira (Environmental Toxins). Sumu hizo unaweza kuzipata kwa kuvuta hewa chafu, kunywa maji au chakula kichafu (chenye sumu).


Unaweza kunywa maji, kula chakula au kuvuta hewa yenye sumu bila wewe kujijua. Hii inatokana na ukweli kwamba baadhi ya dawa zinazotumika kuulia wadudu (pesticides) kwenye mboga tunazokula zina kemikali za sumu au baadhi ya dawa zinotumika kusafishia maji zina kemikali za sumu. Vilevile ulaji holela wa dawa za kutibu maradhi unaweza kusababisha sumu mwilini.

Aina ya pili ya sumu ni ile inayojitengeneza yenyewe mwilini kutokana na mfumo wa usagaji chakula (Metabolic Toxins). Wataalamu wanatueleza kuwa chembechembe hai za mwili hujikuta zikitengeneza sumu katika mchakato wake wa kawaida wa usagaji chakula.

SUMU HUTOKAJE MWILINI
Sasa umefahamu kuwa hauko salama na sumu. Kila wakati, kwa njia moja au nyingine, unaingiza sumu mwilini. Lakini habari njema ni kwamba mwili umepewa uwezo wa kutoa sumu hizo na kujisafisha wenyewe (automatically).

Kwa kawaida, sumu zote hukusanywa na kutolewa mwilini kwa njia ya mkojo, haja kubwa, jasho, makamasi na hata unapokohoa au kupiga chafya huwa ni njia moja wapo ya mwili kujisafisha.

NJIA NYINGINE YA KUTOA SUMU ZAIDI
Ili kuusaidia mwili kuondoa sumu zote mwilini na kujisafisha, mambo makuu manne hayana budi kuzingatiwa na kuwa sehemu ya staili ya maisha yako.

1. Hakikisha unaishi katika mazingira yenye hewa safi ili kujiepusha na uvutaji wa hewa chafu.

2. Hakikisha unapata muda wa kupumzisha mwili na akili kadri iwezekanavyo.

3. Hakikisha mwili haukaukiwi maji kwa kunywa maji ya kutosha kila siku na matunda yenye maji maji.

4. Jiepushe kuishi katika mazingira yenye hewa chafu ili kuuepusha mwili wako kudhurika kwa sumu, ndani na nje ya mwili.

ONDOA SUMU ANGALAU MARA MOJA KWA MWAKA
Jiwekee utaratibu wa kuondoa sumu mwilini kwa kufanya ‘dayati’ maalum, angalu mara moja kwa mwaka. Moja ya njia zinazoaminika katika utoaji wa sumu mwilini, ni ulaji wa matunda, mboga na juisi za matunda kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Katika kipindi hicho cha siku tatu, hutakiwi kula aina yoyote ya chakula au kinywaji zaidi ya matunda, mboga za majani na juisi za matunda au mboga, zilizotengenezwa zikiwa ‘fresh’.

Miongoni mwa matunda na mboga zinazoshauriwa kuliwa ni pamoja na maparachichi, nyanya, vitunguu, matango, karoti, kabichi, tufaha, matikitimaji, ndizi, mapapai, zabibu, nazi na machungwa.

Fanya zoezi la kusafisha mwili kwa kula ‘dayati’ iliyotajwa hapo juu, japo mara moja kwa mwaka, ili uuweke mwili wako safi na hivyo ujiepushe na maradhi hatari kama vile saratani na magonjwa ya moyo.

Chanzo:Global Publishers

No comments: