MWENYEKITI mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Amos Sagara amewaomba viongozi wa kiroho kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani katika wilaya hiyo ambayo imekuwa ikukumbwa na machafuko ya koo mara kwa mara.
Sagara ambaye pia ni diwani wa kata ya Sirari (CCM) alitoa ombi hilo juzi wakati akikabidhi gari jipya kwa Mchungaji wa Kanisa la PEFA, lililopo katika kijiji cha Gwitiro, John Nyamataga.
Gari hilo aina Hilux Picup limenunulia na washirika wa kanisa hilo kupitia kikundi chao cha kanisa hilo cha Inuka Uangaze.
“Ninawaomba wachungaji waendelee kuhubiri amani ili watu wetu waondokane na vita vya koo na tuwekeze zaidi kwenye elimu ya vijana wetu,” alisema Sagara ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo.
Alielezea kuridhishwa na amani iliyopo kwa sasa katika wilaya hiyo, jambo ambalo alisema litasaidia kuharakisha maendeleo ya wananchi. “Sasa hakuna vita, Tarime ndio maana tunawanunulia wachungaji magari.
Huu ni mfano mzuri ambao unapaswa kuigwa na makanisa mengine yote,” alisema. Mwenyekiti huyo alichangia zaidi ya Sh laki tano ikiwa ni sehemu ya gharama za uendeshaji wa gari hilo ambalo thamani yake haikufahamika mara moja.
Kwa upande wake Mchungaji Nyamataga na viongozi wengine wa kiroho, walitumia sehemu ya alfa hiyo kumuombea Sagara ili Mungu amtungulie wakati anatakeleza majukumu yake katika kuhudumia wananchi wa Tarime.
Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, imelazimika kuanzisha Kanda Maalumu ya Kipolisi katika Wilaya ya Tarime ili kukomesha mapigano ya koo ambayo yamekuwa yakigharimu maisha ya watu wasio kuwa na hatia katika miaka ya hivi karibuni.
Wilaya hiyo pia ni maarufu katika kilimo cha bangi na kwa mujibu wa taatrifa za Polisi, imekuwa ikigubikwa na matukio ya wizi wa ng’ombe ambayo yaanambatana na matumizi ya risasi za moto mara kwa mara.
Chanzo:Habari Leo
No comments:
Post a Comment