ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 10, 2011

MKUTANO KWA WATANZANIA,DMV

Watanzania wenzangu DMV usisahau kujiandikisha kwa ajili ya mkutano wetu DMV utakaofanyika january 29,2011 huu mkutano ni muhimu sana kwa Jumuiya yetu.
Madhumuni ya mkutano huo yatakuwa yafuatayo:-
(i) Balozi kujitambulisha rasmi kwa Watanzania washio katika eneo la Washington DC Metro.
(ii) Kuchagua na kuunda kamati ya muda itakayoandaa katiba mpya ya jumuiya na hatimaye kuitisha na kusimamia uchaguzi mkuu wa Jumuiya mpya ya watanzania waishio Washington DC Metro.
(iii) Masuala mengineyo muhimu yatakayojitokeza yanayohusu watanzania waishio hapa Washington DC Metro.
MAHALI:
Hollywood Ballroom - 
2126 Industrial Pkwy, 
Silver Spring-MD 20906 
(Sehemu ya maegesho ipo yakutosha)

MUDA:
Saa 10.30 jioni (Tafadhali zingatia muda)

Ili kukamilisha maandalizi ya mkutano huo, unaombwa kujiandikisha Ubalozini kwa kuandika jina lako hapo chini.Sehemu hii ni salama(secure)nataarifa zako zitalindwa.
Maelezo yako ni kwa lengo la kufanikisha mkutano huo nakujenga takwimu kuhusu Diaspora ya Watanzania. Taarifa zote zitahifadhiwa kwa siri. 
Kwa kujiandiskisha BOFYA HAPA

No comments: