ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 7, 2011

‘Kufanya biashara usiku kutapunguza msongamano’-Mwananchi

Dk Cyril Chami
Festo Polea
SERIKALI imesema wafanyabiashara wanaoendelea kufanya biashara majira ya usiku katika eneo la Kariakoo kutasaidia kupunguza msongamano wa watu na foleni za barabarani.

lakini zoezi hilo ili lifanikiwe linatakiwa kuachiwa jeshi la polisi kanda ya Dar es salaam ili lijipange  jinsi ya kufanikisha ulinzi katioka eneo hilo.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masomo, Dk Cyril Chami, alitoa kauli hiyo, mwishoni mwa wiki wakati akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua ni jinsi gani, serikali imejipanga kuhakikisha huduma, zinaendelea katika eneo la Kariakoo hata majira ya usiku.

 “Hakuna anayekataza shughuli za biashara, zisiendelee Kariakoo majira ya usiku, isipokuwa watu wanafunga maduka yao kutokana na kuhofia vitendo viovu vikiwemo wizi na ujambazi, lakini kwa kuwa Kamanda Kova alilizungumzia hilo, serikali inapongeza mpango huo, na polisi wanapaswa kujipanga  ili watu wasikumbwe na matatizo ya kuvamiwa,’’ alisema.

Dk Chami alisema endapo polisi wataimarisha ulinzi  katika eneo hilo, serikali itazidi kuliunga mkono kwa kuwa lengo hilo, ni zuri.
Awali jeshi hilo, Kanda ya Dar es salaam iliweka ulinzi katika sikukuu ya Iddi katika eneo la Kariakoo na hivyo kufanikiwa katika mpango huo.

Kamanda wa kanda hiyo, alisema alikutana na wafanyabisahara wa eneo hilo, ili kupanga mikakati ya kuweka askari wa kutosha majira ya usiku kwa lengo la kuendelea na biashara.

Alisema angekutana na wamiliki wa maduka katika eneo hilo ili kupanga jinsi ya kuweka ushirikiano kati yao na jeshi hilo ili kuzuia hatari za kuvamiwa na watu wasiokuwa na nia njema.

No comments: