ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 5, 2011

Jumuiya ya OMCT yataka Bush akamatwe kwa kutesa wanadamu

Jumuiya Kimataifa ya Kupiga Vita Mateso imeitaka Uswisi kuanzisha uchunguzi wa jinai dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush anayetazamiwa kuitembelea nchi hiyo tarehe 12 mwezi huu wa Februari, kwa uwanja huo.
Jumuiya ya Kupiga Vita Mateso (OMCT) imemwandikia barua Rais wa Uswisi na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo ikiwataka viongozi hao kuanzisha uchunguzi wa makosa ya jinai dhidi ya George Bush kwa kuhusika na mateso dhidi ya binadamu. Mkurugenzi wa jumuiya ya OMCT Eric Sottas amesema Uswisi inapaswa kufungua mashtaka dhidi ya watu wote wanaoruhusu, kushiriki au kula njama ya kufanya mateso na manyanyaso dhidi ya binadamu. Eric Sottas amesisitiza kuwa hakuna sheria inayowapa kinga marais wa zamani katika uwanja huo. Jumuiya ya kupunga mateso ya OMCT imesema kuna ushahidi madhubuti unaoonyesha kwamba serikali ya Bush ilitekeleza mateso kwa kiwango kikubwa na kwamba Bush mwenyewe amekiri kuwa ameruhusu matumizi ya mateso dhidi ya baadhi ya watuhumiwa wa ugaidi.
Bush anatazamiwa kuwasili Uswisi siku kadhaa zijazo ambako amealikwa na jumuiya moja ya Kiyahudi, safari ambayo inakabiliwa na upinzani mkubwa wa jumuiya za kutetea haki za binadamu.tuhuma za kuhusika na mateso dhidi ya binadamu na kukiuka makubaliano ya kimataifa katika 

1 comment:

Anonymous said...

absolutely,he should