.jpg)
Msafara wa mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, umepata ajali ambayo imeua mtu mmoja alifariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa.
Ajali hiyo iliyotokea jana maeneo ya Ruvu mkoani Pwani, ilihusisha basi la abiria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,
Absalom Mwakyoma, alisema basi la Moro Best lenye namba T.237 lililokuwa likielekea Dar es Salaam kutoka Mpwapwa liligonga basi dogo Toyota Hiace maarufu kama kipanya lenye namba T.310 BBC, ambalo lilikuwa limeegeshwa pembeni ya barabara.
Alisema baada ya kugonga gari hilo lilienda kugonga gari lenye namba T. 849 AKT lililokuwa kwenye msafara wa Mama Kikwete.
Alisema gari lililokuwa limembeba Mama Kikwete halikuhusika katika ajali hiyo na alifika Dar es Salaam akiwa salama.
Alisema watu sita waliokuwa katika basi dogo walijeruhiwa na dereva wa gari lililokuwa kwenye msafara huo aliyetambuliwa kwa jina la Ramadhani Mkoma, alikufa papo hapo na majeruhi walikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu.
Mwakyoma alimtaja dereva wa basi la Moro Best kuwa ni Abdul Majeshi, ambaye alikimbia mara baada ya ajali hiyo.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment