Maelfu ya wageni wanaofanya kazi nchini Libya kwa sasa wanahangaika kutafuta njia ya kuondoka nchini humo.
Kuanzia Marekani hadi China, serikali zinatafakari njia za kuwanusuru raia wake walioko nchini humo.
Inakadiriwa kuwa kuna takriban raia elfu ishirini na watano wa Uturuki walioko Libya.
Serikali yao imetuma meli na merkebu za kijeshi, huku mataifa kama Ufaransa na Uholanzi zikiwa zimetuma ndege za kijeshi.
Uingereza imetuma ndege ya kukodi wakati wizara ya mambo ya kigeni ikiahidi kutuma ndege nyingine.
Serikali ya Ugiriki inasema kuwa inatuma meli tatu za kibiashara kwenye pwani ya mji wa Benghazi, na kuahidi kusaidia kusafirisha raia 30,000 wa Uchina.
Pamoja na juhudi hizo kuna wahudumu wengine wengi kutoka mataifa kama Bangladesh, Vietnam na Ufilipino, ambao serikali zao hazijatangaza mipango madhubuti ya kuwaokoa raia wake.
Wakati huo huo, Ubalozi wa Libya nchini Austria umeishutumu serikali kwa kutumia jeshi na ndege zake kushambulia raia wake.
Haya ni katika mfululizo wa shutuma za wanabalozi wa Libya wakijitenga na serikali ya Kanali Gaddafi.
No comments:
Post a Comment