Advertisements

Tuesday, February 15, 2011

SHUKRANI


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar anapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Watanzania wote waliohudhuria mkutano wake pamoja nao uliofanyika Januari 29, 2011 ambao ulikuwa wa mafanikio makubwa. Matokeo ya mkutano yalikuwa kufanikisha kuchaguliwa kwa KAMATI YA KATIBA ya kuandaa katiba mpya kwa madhumuni ya kuhuisha tena umoja wa Watanzania waishio Washington Metro.

Aidha, Mhe. Balozi anawashukuru na kuwapongeza wapasha habari wote ambao walisambaza taarifa za mkutano  wakiwepo Lucas Mukami wa Vijimambo Blog, Sunday Shomari wa Sunday Shomari Blog, Abuu Shatri wa Swahili Villa Blog, na Bandio Mubelwa wa Changamoto Yetu Blog. Mhe. Balozi anamshukuru pia Ernest Kessy na Kampuni yake ya Metro Tyres kwa kuuzawadia Ubalozi matairi manne kwa ajili ya gari la huduma. Mhe. Balozi amefarijika sana na moyo ulioonyeshwa na Watanzania wenzake ambao umempa nguvu zaidi ya kushirikiana nao kwa kila kitu siku zote.

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON D.C.


No comments: