Uchaguzi mkuu wa Urais na Wabunge uliofanyika Uganda mwishoni mwa juma lililopita umemalizika kwa Museveni kuibuka tena na ushindi. Lakini kwa upande mwingine kidogo umeleta hasara kutokana na karibu nusu ya mawaziri wake kutupwa nje na wabunge wengi waliosimama wanaojitegemea, japo wanaegemea NRM ndio wameshinda.
Mbali na uchaguzi wa Urais lakini pia mwishoni mwa juma kulifanyika uchaguzi wa wabunge. Matoke yanafika polepole Kampla kutoka mikoani ya uchaguzi ulivyokuwa.
Mawaziri takriban 19 wamepoteza viti vyao. Miongoni mwa hao ni Waziri wa Elimu Bi Bitamazire, wa Teknonolojia ya habari- ICT Aggrey Awor pamoja na Waziri wake mdogo, Alintuma Nsambu, Wazir wa Maadili Nsaba Buturo katupwa nje, ilahli Waziri wa Ardhi Omara Atubo nae nje.
Vijana wengi wameingia bungeni mara hii kuliko ilivyokuwa Bunge lililopita. Kuhusu hilo mbunge wa Uganda katika Bunge la Afrika Mashariki kutoka chama cha NRM Bi Lydia Wanyoto amesema kuwa hilo ndilo walikuwa wakilipigania.
Msemaji wa NRM Ofono Opondo amesema chama chake kinaweza kikapata wabunge 75 katika bunge la wajumbe 300 na zaidi, akiongeza ni NRM tu ambayo ilikuwa na mgombea karibu katika kila wilaya zote 112.
Ameongeza kuwa eneo la kaskazini ambako Museveni amekuwa akipata asilimia 17 tu kutokana na vita vya muda mrefu, sasa amepata asilimia 41 na kuongeza wamefaulu kumung’oa kiongozi wa upinzani.
No comments:
Post a Comment