ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 10, 2011

Wachaga waongoza kwa kutumia benki! ehh -darhotwire

Utafiti umebaini kwamba Mkoa wa Kilimanjaro, unaongoza kwa kutumia huduma za kibenki kwa asilimia kubwa na kuwa na idadi kubwa ya watu waoelewa na kudhubutu kuanzisha biashara mbalimbali.

Kwa mujibu wa utafiti huo, Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa unaoongoza kwa kuwa na uelewa mkubwa katika Kanda ya Kaskazini kuhusiana na huduma za kifedha na kufuatiwa na Arusha, na Manyara.

Hayo yalisemwa jana na mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa masuala ya uchumi na kijamii Tanzania (ESRF), Dora Semkwiji wakati akiwasilisha taarifa hiyo, katika warsha ya mahitaji na vikwazo vya kupata huduma za kifedha nchini.

Semkwiji alisema wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, wamekuwa na uelewa mkubwa katika masuala ya fedha kwa kuwa wanazingatia mafunzo na kutumia uzoefu walionao katika shughuli za kibiashara tangu wakiwa wadogo.

Alisema taarifa hizo, zimepatikana baada ya ESRF kufanya utafiti katika kanda zote Tanzania na kubaini, uliopewa jina la Fin scope na kusisha sampuli ya watu 7,680 kuoanishwa na Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS).

Alisema utafiti huo, ulilenga zaidi katika upatikanaji na vikwazo kuhusu huduma za kibenki nchini na ni jinsi gani wananchi wana uelewa wa matumizi ya huduma za kibenki.

Akiwasilisha taarifa hiyo, alisema Kanda ya Kaskazini inaongoza kwa kutumia huduma za kibenki kwa asilimia kubwa na kutumia mikopo kwa kiasi kikubwa zaidi.

1 comment:

Anonymous said...

Duh hongereni wachaga na sie wazaramo sijuwi mwakani tutakua wangapi???...........lol.Meya seattle wa.