Dk Lucy Nkya
IMEELEZWA kuwa hadi sasa hakuna dawa iliyodhibitishwa kitaalamu kuwa inaweza kutibu ugonjwa wa kisukari na kwamba waganga wanaojitangaza mitaani na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa wanatibu ugonjwa huo ni walaghai.
Akijibu swali bungeni jana Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya alisema kuwa hadi sasa tafiti za kitaalamu zilizofanywa nchini na duniani zimeonyesha kuwa dawa zote zilizopo pamoja na za asili zina uwezo wa kudhibiti ugonjwa usisababishe madhara zaidi lakini hazina uwezo wa kuponyesha kabisa.
“Katika mfumo wa tiba asili,kuna dawa nyingi zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa kisukari mwilini kama ilivyo katika mfumo wa tiba za kisasa.Wizara kupitia Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR) na Taasisi ya tiba asili ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba ya Jamii Mhimbili ,hufanya tafiti mbalimbali za dawa asili zinazosadikiwa kutibu magojwa mbalimbali ikiwemo kisukari.
Matokeo ya tafiti hizo hayajaonyesha dawa yoyote ya asili yenye uwezo wa kutibu kisukari,”alisema Dk Nkya.
Alisema waganga wa tiba asili wanashauriwa kuwasiliana na taasisi za utafiti ili kupata maelezo yanayohusu ufanisi na usalama wa dawa zao wanazozitumia kudhibiti ugonjwa wa kisukari na magojwa mengine badala ya kutangaza dawa hizo pasipo tafiti za kitaalamu.
Dk Nkya ambaye alikuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu (CCM) Kidawa Hamis aliyetaka kujua tamko la serikali kuhusiana na wimbi la waganga wa tiba asilia wanaojitangaza kutibu ugonjwa wa kisukari,alisema kuwa dawa inapotangazwa kwenye vyombo vya habari lazima iwe imefanyiwa utafiti wa kitaalamu na kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu kinyume chake ni uvunjwaji wa sheria.
Alisema waganga wa tiba asili hawapaswi kukiuka sheria namba 23 ya mwaka 20002 kuhusu tiba mbadala na kanuni zake, hivyo kabla ya kutangaza hizo dawa zao kwa umma wanapaswa wawasiliane na waganga wakuu wa wilaya na mikoa ili taratibu za kuzifanyia dawa hizo utafiti wa kisayansi ufanyike.
Zaidi Dk Nkya aliitahadharisha jamii kuhusiana na dawa hizo asili zinazotajwa kutibu ugonjwa wa kisukari kuwa hazitibu zaidi ya baadhi kudhibitika kuudhibiti ugonjwa hivyo na kwamba wananchi wajenge tabia ya kwenda kuchunguza hali ya afya zao mara kwa mara ili kuwezesha kudhibiti ugonjwa mapema

No comments:
Post a Comment