Na Mwandishi Wetu
TUHUMA nzito za ubakaji na kumpachika mimba denti mwenye umri wa miaka 13 (jina tunalihifadhi) zinazomkabili Mkurugenzi na Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki Lwambo huenda zikampeleka miaka 30 jela endapo zitathibitika ni kweli.
Choki ‘Mzee wa Farasi’ anatuhumiwa kumbaka na kumsababishia ujauzito msichana huyo yatima, huku ikidaiwa kwamba ana uhusiano naye wa muda mrefu.
Kwa mujibu wa wanasheria waliozungumza na gazeti hili, tuhuma zinazomkabili Choki ni nzito na endapo itathibitika kwa asilimia 100 kwamba alitenda kosa hilo, atakwenda jela kwa kifungo kisichopungua miaka 30.
Aidan Kombo ambaye ni mhitimu wa shahada ya sheria ngazi ya uzamili alisema: “Inategemea mazingira ya tukio lakini ikithibitika ni miaka 30 lakini hakimu anaweza kwenda zaidi ya hapo.”

Aliongeza: “Kama mtuhumiwa atafanya kosa hilo kwa nguvu au vitisho, kama msichana au mwanamke atakuwa hana akili timamu au atakuwa amelewa, mtuhumiwa anaweza kuhukumiwa adhabu kali zaidi. Usishangae tukasikia kifungo cha maisha.”
Wanasheria wengine waliozungumza na Ijumaa Wikienda, Albert Ndege na Sabatian Mafungo hakuwatofautina na Kombo katika kueleza tukio hilo.
Choki alifunguliwa kesi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam kwa jalada lenye namba OB/ RB/3840/ 2011.
Katika kesi hiyo, Choki anadaiwa kuwa na uhusiano na binti huyo aliyezaliwa mwaka 1997 kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa makosa ya kijamii, hatia ya kufanya mapenzi na mtu aliye na umri wa chini ya miaka 18 huhesabika ni ubakaji.
Maelezo ya binti huyo ambaye kwa sasa anayeishi na bibi yake Ubungo, River Side, Dar yanadai kwamba hajawahi kukutana na mwanaume mwingine tangu alipokutana na mwanamuziki huyo, kwa hiyo ujauzito alionao ni wa Choki.
Hata hivyo, akizungumza na redio moja hivi karibuni jijini Dar, Choki alisema, kesi hiyo ni fitina zinazopikwa na maadui zake ili kumtibulia mipango ya uzinduzi wa albamu ya bendi yake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ASET, Asha Baraka anayemiliki Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ alisema, matatizo ya Choki yamemuuma kama mdau wa muziki.
“Kuna haja ya kukaa, tuone jinsi ya kushirikiana ili kusaidiana hili,” alisema Asha.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment