Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limebaini kuwepo kwa
vitendo vyaa wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kujihusisha na
masuala ya Siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo
za vilabu na wadhamini wa Ligi.
Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is neutral in matters of
politics and religion. Discrimination of any kind against a country,
private person or group of people on account race, skin colour, ethnic,
national or social origin, gender, language, religion, political opinion
or any other opinion, wealth, birth or any other status is strictly
prohibited and punishable by suspension or expulsion.”
Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “ Hairuhusiwi kwa
mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia yeyote tangazo
au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni maalum bila
idhini ya TFF/TPLB”.
TFF inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo
viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni
marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za
kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track
suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa stars au za
washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.
Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa.
Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni
za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa
ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya katiba za TFF na
FIFA.
No comments:
Post a Comment