Mhe. Pinda akihutubia |
Mfalme
wa Lesotho Mhe. Letsie III ambaye nae alihudhuria mkutano huo
akihutubia wadau mbalimbali na wageni waalikwa walioshiriki katika
mkutano huo (hawapo pichani). |
Balozi wa Tanzania anayeiwakilisha nchini Lesotho, Mhe. Radhia Msuya (kulia) akifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo |
Wageni waalikwa |
Wadau mablimbali wakifuatilia hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na viongozi ho
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe naye alitoa Hotuba yake wakati wa Hafla hiyo |
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau mbalimbali katika meza kuu |
Tanzania
imeendelea kuunga mkono jitihada za kitaifa na kimataifa katika
kuhakikisha usalama wa chakula pamoja na lishe bora yenye virutubisho
muhimu hususan kwa watoto wadogo, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha
inapatikana kwa maendeleo endelevu ya taifa.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Mizengo Pinda alipozungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano
wa Kilele wa Dunia kuhusu masuala ya Chakula na Lishe uliofanyika
kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha hivi karibuni.
Mhe.
Pinda alisema kuwa jitihada hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimeelekezwa
katika kuhamasisha unyonyeshaji wa watoto wachanga na kutumia vyakula
vyenye virutubisho kwa watoto wa kuanzia miezi sita hadi mwaka mmoja
umesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo vitokananvyo na ukosefu wa
chakula bora na utapiamlo.
Aliongeza
kuwa Tanzania imekuwa na program mbalimbali kwa vipindi tofauti katika
kupambana na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa vyakula vyenye
virutubisho na madini muhimu ikiwemo program ya kuongeza madini joto
kwenye chumvi iliyozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali
Hassan Mwinyi mapema mwaka 1990 ili kupambana na magonjwa
yanayosababishwa na upungufu wa madini hayo mwilini ikiwemo ugonjwa wa
goiter ambao ulienea nchini miaka ya 1980.
Aidha,
mwaka 2013 Serikali ilizindua Program ya Kitaifa ya Uboreshaji wa
Chakula ambapo virutubisho muhimu viliongezwa kwenye vyakula vinavyoliwa
zaidi katika jamiii ya Watanzania ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 25
ya watu wanatumia unga wa ngano na mahindi pamoja na mafuta ya kupikia
yaliyoongezwa virutubisho vyenye madini na vitamin muhimu kama chuma,
zinki na Vitamini A na B12.
“Kwa
upande wa Tanzania jitihada nyingi za kuhakikisha suala zima la
upatikanaji wa chakula bora ili kuwawezesha wananchi kuwa na afya bora
ili kuchangia katika maendeleo ya taifa lao zimefanyika. Miongoni mwa
jitihada hizo ni pamoja na kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama
kwa watoto wachanga, kuzinduliwa kwa Mkakati wa Taifa wa Lishe wa
miaka mitano hapo mwaka 2011 ambao lengo lake kubwa ni kuhamasisha
matumizi ya vyakula vyenye virutubisho” alisema Mhe. Pinda.
Aidha,
alieleza kuwa kwa sasa Serikali kupitia Mamlaka za Serikali za mitaa
imeweka mkazo kuhakikisha huduma ya uboreshaji vyakula kwa kuongeza
virutubisho muhimu inapelekwa katika maeneo ya vivijini ambapo zaidi ya
asilimia 70 ya Watanzania wanaishi huko.
“Mifumo inaandaliwa ili kuhakikisha mamalaka hizi zinafanikisha uboreshaji wa vyakula ikiwemo unga wa nafaka unaozalishwa katika mashine za kawaida na mafuta ya kula yanayotengenezwa na wananchi vijijini yanaboreshwa” alisisitiza Mhe. Pinda.
“Mifumo inaandaliwa ili kuhakikisha mamalaka hizi zinafanikisha uboreshaji wa vyakula ikiwemo unga wa nafaka unaozalishwa katika mashine za kawaida na mafuta ya kula yanayotengenezwa na wananchi vijijini yanaboreshwa” alisisitiza Mhe. Pinda.
Katika hatua nyingine Mhe. Pinda alisifu na kuwashukuru waandaaji wa mkutano huo kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji kwani
ni wakati muafaka ambapo kampeni hii ya dunia itasaidia kuhamasisha pia
wananchi na wawekezaji katika sekta ya chakula hapa nchini na hatimaye
kuleta matokeo endelevu katika lishe na usalama wa afya ya jamii kwa
ujumla.
Pia
alisema kuwa kwa vile mkutano huo umewashirikisha watu kutoka
Serikalini, wafanyabiashara, taasisi za kiraia, mashirika ya kimataifa,
wanazuoni na washirika wa maendeleo ana imani kubwa kuwa utaainisha
mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya baadaye kuhusu uboreshaji wa
afya ya jamii zetu kwa maendeleo endelevu.
Mkutano
huo ambao ulihudhuriwa pia na Mfalme Letsie III kutoka Lesotho ambaye
pia ni Kiongozi wa kuhamashisha matumizi ya chakula bora na lishe wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika, alisema kwamba lishe bora ni msingi wa
maendeleo ya kiuchumi kwa kila taifa. Kwamba kuwekeza kwenye lishe ni
muhimu ili kupunguza umaskini kwa kuhakikisha kila mwanajamii anachangia
kwa taifa lake.
Alieleza
kuwa Mkakati wa Lishe wa Kanda ya Afrika kwa kipindi cha kuanzia mwaka
2015-2025 uliozinduliwa mwezi Julai mwaka huu kuwa unasisitiza
ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika kuboresha lishe ikiwemo sekta
binafsi ambapo alitoa tahadhari kwa wafanyabiashara kutotumia fursa hii
kujitengenezea faida kubwa kwa bidhaa watakazozalisha badala ya
kuangalia afya za watu kwanza. Pia mapendekezo kuhusu njia bora za
uchangiaji mpango wa lishe Afrika yalijadiliwa.
“Natoa
tahadhari kwa wenzetu wa sekta binafsi kuhakikisha afya ya mtu inapewa
kipaumbele na kuhakikisha ari ya kujipatia faida haihatarishi afya ya
mtu yeyote”alisisitiza Mfalme Letsie III.
Pia
aliongeza kuwa, Kamisheni ya Umoja wa Afrika na nchi wanachama
zinatambua kwamba Serikali pekee haziwezi kutatua changamoto ya lishe
duni inayolikabili Bara la Afrika bali jitihada za wadau wote muhimu
zinahitajika ikiwemo sekta binafsi hususan kampuni zinazozalisha na
kutengeneza vyakula, Mashirika ya Kimataifa, taasisi za kiraia na
wanazuoni wanatakiwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya lishe bora kwa
kila mtu.
Awali
akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe alisma kuwa amefarijika mkutano wa
kwanza kuhusu masuala ya chakula na lishe umefanyika nchini na kwamba
mada zitakazojadiliwa wakati wa mkutano huo zitaziwezesha nchi za Afrika
ikiwemo Tanzania kuangalia namna bora ya kuboresha lishe kwa ajili ya
kujiletea maendeleo.
Mkutano
wa Kilele wa Dunia kuhusu uboreshaji wa Chakula na Lishe
uliowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya kimataifa,
serikali, wanazuoni, washirika wa maendeleo na sekta binafsi umefanyika
Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 Septemba, 2015.
No comments:
Post a Comment