
Tunashauriwa kuwasiliana mara kwa mara na wapenzi wetu, lakini si wote tunaofahamu mawasiliano yanayoweza kuharibu uhusiano wa kimapenzi.
Leo tutaangalia aina tatu za mawasiliano hatari kwenye mapenzi.
1. MAWASILIANO YA KUENDESHA
Utafiti unaonesha kuwa, asilimia kubwa ya watu hasa wanaume huwasiliana na wenza wao kwa kutumia aina ya mawasiliano ya kulazimisha mambo wanayotaka yafanyike. Utakuta mtu anapiga simu au kuongea na mwenzake huku akiwa ameshajenga msimamo wake juu ya suala fulani analotaka lifanyike.
Leo tutaangalia aina tatu za mawasiliano hatari kwenye mapenzi.
1. MAWASILIANO YA KUENDESHA
Utafiti unaonesha kuwa, asilimia kubwa ya watu hasa wanaume huwasiliana na wenza wao kwa kutumia aina ya mawasiliano ya kulazimisha mambo wanayotaka yafanyike. Utakuta mtu anapiga simu au kuongea na mwenzake huku akiwa ameshajenga msimamo wake juu ya suala fulani analotaka lifanyike.
Sura ya mawasiliano ya aina hii huwa haitoi nafasi kwa upande wa pili kuonesha hisia na maamuzi yao.
“Mi nimekuja hapa kukuchukua, sitapenda kabisa niondoke bila kuogozana na wewe...hata kama hujaaga we twende tu.” Kifupi haya si mawasiliano ya kimapenzi, ni amri ya mtu.
2. MAWASILIANO YA KUDANGANYA
Hii ni moja kati ya aina hatari zaidi za mawasiliano ambayo huharibu haraka uhusiano. Uongo na utiaji chumvi wa mambo husababisha machafuko na maumivu makali kwenye mapenzi.
Kuna watu hodari sana wa kudanganya kwenye mapenzi, utakuta jambo liko wazi lakini wanatumia muda mwingi kuwasiliana na wenzao kwa lengo la kusema uongo.
Tabia hii inatajwa kuharibu karibu nusu ya mapenzi na hivyo kuingizwa katika orodha ya pili ya mawasiliano hatari katika uhusiano yanayotakiwa kuepukwa haraka.
Kinachotakiwa hapa ni kwa wapenzi kuwa waadilifu. Ukipigiwa simu kuulizwa uko wapi, taja sehemu sahihi, usitunge. Mpenzi wako akibaini unadanganya atakuchukia na kutopenda kuwa na wewe maishani mwake.
3. MAWASILIANO YA ‘NDUMILAKUWILI’
Mawasiliano haya ni yale ambayo mtu anaweza kusikika akisema, anampenda mwenzake kumbe ana maanisha anamchukia.
Wapo watu wengi sana ambao kwao ni rahisi kuahidi kuwa watatenda hili na lile kumbe hawamaanishi hivyo. Aina hii ya mawasiliano inafanana sana na ile ya udanganyifu, lakini mawasiliano haya huwa na sura mbili zinazofanana kwa wakati mmoja.
Anaweza kuja mpenzi wako akiwa kavaa sura ya matatizo, akajaribu kukulilia shida mpaka ukaamini na kuamua kumsaidia, kumbe alichokuwa akifanya ni kukuweka sawa ili apate fedha ya kwenda baa kunywa au kufanya mambo yake.
“Nimekuja, yaani baba ... mtoto anaumwa sana, nataka nimpeleke hospitali.”
Baada ya muda ukifuatilia kauli hii utabaini kuwa mtoto haumwi ila mama alikuwa amevaa sura mbili ili apate pesa ya mchezo. Mawasiliano ya aina hii hayafai kwenye mapenzi.
Baada ya kusema hayo ni vyema nikaeleza kwamba siku zote mawasiliano yatabaki kuwa nguzo muhimu kwenye mapenzi, lakini haitakiwi kabisa kuwa na aina ya mawasiliano niliyotaja hapo juu.
Kwa leo naomba niishie hapa ukiwa na maswali tafadhali nipigie au tukutane kwenye Mtandao wa Facebook, kujiunga nami andika jina la Richard Manyota.
No comments:
Post a Comment