
Ndege ya American Airline 737 ambayo ilikua imebeba abiria 134,ilibidi itue kwa dharura Dayton,Ohio baada ya abiria wake kuanza kuugua ghafla na kupelekea kuzimia kwa abiria wawili.
Muda mfupi baada ya kuruka Ijumaa asubuhi April 1,2011 ndege # 547 Reagan National Airport iliyopo Washington,DC kuelekea Chicago,wahudumu wawili wa ndege hiyo waliripotiwa kwamba walianza kujisikia kizunguzungu,ndipo pilot alishusha Oxygen Masks.
Abiria Sita walipata matibabu ya huduma ya kwanza mara tu waliposhuka kwenye ndege uwanjani hapo,Dayton,OH,na Abiria wengine wawili ilibidi wakimbizwe Hospitali.
No comments:
Post a Comment