
Na Luqman Maloto
Karibu msomaji wangu. Uwanja wetu ni ule ule na maudhui ni yale yale, sisi bado hatujajivua magamba. Inampendeza Mungu kila upande.
Mapenzi yana uwanja mpana ingawa sura zake ni mbili.
Amani kwa maana ya pale ambapo mambo yametulia na migogoro kwenye eneo ambalo wawili wanaopendana hawana furaha wala maelewano.
Mada hii itakuwa na lengo moja tu la kuponya wale wote wanaoishi kwenye mapenzi yasiyo na amani. Yale yanayoashiria kifo cha mapema na kuwafanya wabadili uelekeo.
Karibu msomaji wangu. Uwanja wetu ni ule ule na maudhui ni yale yale, sisi bado hatujajivua magamba. Inampendeza Mungu kila upande.
Mapenzi yana uwanja mpana ingawa sura zake ni mbili.
Amani kwa maana ya pale ambapo mambo yametulia na migogoro kwenye eneo ambalo wawili wanaopendana hawana furaha wala maelewano.
Mada hii itakuwa na lengo moja tu la kuponya wale wote wanaoishi kwenye mapenzi yasiyo na amani. Yale yanayoashiria kifo cha mapema na kuwafanya wabadili uelekeo.
Wanaweza kuanza kuheshimu kile kilichowaunganisha. Yaani kuufanya ‘uspesho’ wao uwe na maana. Ikiwa hivyo, basi watakuwa wanaondokana na jinamizi la kifo cha haraka. Hapa si utani, inahitaji utulivu kujua.
Msongo wa mawazo kila siku au mara kwa mara, husababisha mwili kushindwa kufanya kazi sawasawa. Athari kubwa huelekea kwenye moyo ambao ndiyo injini ya mwili wa binadamu.
Mapenzi ndiyo kitu namba moja kinachoweza kumfanya mtu awe na msongo mkubwa wa mawazo. Fedha au njia zake ni kichocheo namba mbili lakini kina unafuu wake pale unapopata faraja kutoka kwa mwenzio.
Katika mapenzi hakuna kinachoweza kukupa ahueni zaidi ya kuelewana na yule unayempenda. Yule aliyekuudhi, vinginevyo utakosa utulivu wako. Mapenzi yanaua lakini sizungumzii kunywa sumu.
Nazungumzia athari inayojengeka katika moyo baada ya kutokuwa kwenye maelewano chanya na mwenzi wako. Mwili unakosa upumuaji mzuri, hivyo kutema sumu ndani kwa ndani. Matokeo yake unajiona mgonjwa, kumbe mapenzi.
WAPO WATU WA AINA HII
Mtu hana maelewano na mwenzi wake, moyo unamlazimisha atafute suluhu lakini anakuwa mbishi. Anataka kujionesha kwamba yeye yupo salama na hatishiki kwa lolote.
Saikolojia inakutaka ujitunze usiumizwe. Yaani uwe na tahadhari kutafuta suluhu pale isipostahili lakini kama ishu ni ndogo, iweje isiwekwe mezani na kutafuta ufumbuzi?
Mara nyingi mtu huyu huumia sana baadaye hasa baada ya kugundua ukweli kuwa yule aliyekuwa anamfanyia ‘ushenzi’ amekwishaondoka na pengine hatarudi tena kwake. Amechezea mawe, kapoteza almasi lakini majuto mjukuu!
WAPO NA HAWA
Ipo jamii ya watu ambao hutaka jamii iwaone wao ni ngangari katika mapenzi. Yaani hawawezi kuumia hata wafanywe nini. Wanajidanganya kwa ‘ubishoo’ wao. Kuna kitu utajifunza leo.
Ukweli ni kuwa, hakuna mtu ambaye anaweza kujitenga na maumivu ya moyo pale anapoumizwa na mtu anayempenda. Anaweza kutabasamu akiwa na wewe lakini peke yake ni kilio cha ndani kwa ndani.
Yaani hayupo kwenye hali nzuri na mwenzi wake lakini eti anadhani akisema atachekwa. Amekwishajiaminisha yeye ni ngangari lakini ikae kichwani kuwa mtu wa aina hii ni rahisi kufa.
Si kwa kujinyonga isipokuwa anaweza kuangamia taratibu. Hapa nataka nikupe pointi bora ya maisha kuwa, fanya kila uwezalo kuhakikisha moyo wako unakuwa salama. Usiupe mzigo usio wa lazima.
Maumivu ya mara kwa mara ya kimapenzi ni mzigo mkubwa mno ambao huutwisha moyo wako. Masikini ya Mungu, wenyewe huwa hausemi kwa kutoa sauti ila unapoelemewa maumivu hukurudia mwenyewe.
HAWA NAO VIPI?
Wapo ambao huumizwa wao lakini kutwa kiguu na njia kutafuta suluhu. Haikatazwi kwa maana anatafuta amani ya moyo wake lakini muhimu ni je, huyo anayehangaikiwa yupo vipi?
Ni kujipa mzigo mzito kichwani kubembeleza penzi la mtu ambaye hana hisia na wewe hata kidogo. Bora uumie leo, tafuta faraja kwa watu wako wa karibu, omba kwa Mungu akuvushe salama katika kipindi kigumu.
Anakutenda leo, wewe ndiye unayepigana kutafuta amani irejee na upendo uendelee. Binadamu alivyo na hulka ya ajabu, ukifanya hivyo hawezi kukuona ni mtu bora, isipokuwa ataamini amekupata na huna ujanja, hivyo atarudia yale yale.
Shukuru Mungu kwa namna alivyokuumba. Wewe ni kiumbe kamili, huna upungufu wa aina yoyote, hivyo usikubali mtu mwingine aje auponde moyo wako. Hata siku moja usiruhusu mtu acheze sebene na moyo wako.
Unatakiwa kuwa wa kwanza kujihurumia kwa sababu hayupo atakayehisi maumivu kwa niaba yako. Kumruhusu mtu anayekuumiza mara kwa mara ni sawa na kutonesha kidonda ambacho ni injini ya mwili wako. Moyo!
Itaendelea wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment