ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 17, 2011

Mume atishia kumdai mke wake mamilioni

MKAZI wa Kata ya Matongo, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Stephen Anunda, ametishia kumdai mke wake, Eunice Mroni fidia ya Sh milioni 37.7 baada ya mwanamke huyo kufungua shauri la kumdai talaka katika Baraza la Kisheria. 

Mchanganuo wa fedha hizo kwenye barua yake ya utetezi ('Habarileo' lina nakala yake), unaonesha kuwa alitumia Sh milioni 12.6 kumgharimia mwanamke huyo masomo ya Stashahada ya Uhasibu katika Chuo cha Uhasibu (CBE) Tawi la Mwanza na Sh milioni 6.5 kumgharimia matibabu alipokuwa chuoni hapo.
 

Anunda aliongeza kuwa atamdai pia Sh milioni 16 kama fidia ya udanganyifu wa kumpotezea muda katika suala la ndoa na Sh milioni 2.6 ambazo ni thamani ya ng’ombe wanane aliolipa mahari kwa wazazi wa mwanamke huyo. 

Akizungumza mbele ya Baraza la Kisheria Kata ya Matongo wilayani Tarime Ijumaa, mwanamke huyo alitoa sababu za kudai talaka kuwa ni baada ya kumfumania mume wake huyo mara tatu akiwa katika mazingira ya kimapenzi na mfanyakazi wao wa nyumbani. 

Aidha, katika shauri hilo Na. 24/2011 lililofunguliwa Machi 29, 2011 kwenye Baraza hilo, mwanamke huyo alitaja sababu nyingine ya kudai talala hiyo kuwa ni baada ya kukerwa 
na tabia ya mume wake huyo ya kuendekeza vitendo vya kishirikina.


CHANZO:HABARI LEO

No comments: