ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 3, 2011

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA MAONYESHO YA HARUSI DIAMOND JUBILEE

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, j insia na Watoto, mh.Ummy Ally Mwalim, akipata maelezo katika moja ya mabanda ya maonyesho ya Harusi, yanayoendelea katika ukumbi wa Diamond Jubilee
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim akisaini kitabu cha wageni jana kwenye moja ya mabanda ya maonyesho ya Harusi yanayoendelea katika ukumbi wa Diamond Jubilee



  • Naibu Waziri atembelea Maonyesho ya Harusi Diamond Jubilee.

  • Leo ni siku ya mwisho ya Maonyesho hayo.

  • Wengi wahudhuria kujionea bidhaa, huduma na mapambo ya Harusi.



Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim, jana alipata muda wa kutembelea maonyesho yanayoendelea ya Harusi ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jana jioni.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda yote yanayokadiriwa kuwa zaidi  ya 50 ya wajasiriamali tofauti tofauti wanaojihusisha na masuala ya harusi, Naibu waziri alimsifu muaandaaji wa maonyesho hayo, ambae pia ni mbunifu mahiri wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali kuwa ni mjasiriamali anayejituma na ni mfano wa kuigwa.


“kwa kweli Mustafa amefanya kitu cha kipekee sana, naa ni mfano wa kuigwa, hii inawapa wafanyabiashara husussani wale wa mapabo na keki kuweza kujitangaza na kujifunza mengi wao kwa wao” alisema mheshimiwa Waziri.

Naibu waziri ambae aliweza kupata wasaa wa kubadilishana mawazo na wadau na washiriki wa maonyesho hayo ambao walimpoke kwa furaha huku wakimpa zawadi mbalimbali, aliwasihi na kuwapa moyo wa kuendelea kujituma kwa ari bila kuchoka ili kujipatia kipato na kuwapa huduma wananchi kwa uzuri na usasa zaidi.

Nae muaandaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali, ambae ndie aliyekuwa mwenyeji wa mh. Naibu waziri, alisema kuwa maonyesho ya mwaka huu yamekuwa ni ya aina yake kutokana na kujipanga kwa timu nzima ya uandaaji, huku baadhi ya mambo yakiwa yameongezeka tofauti na mwaka jana.

“mwaka huu sambamba na maonyesho haya, tumeweza pia kuzindua jarida ambalo ni mahususi kwa masuala ya Harusi, hii ni kwa mara ya kwanza Tanzania kuwa na jarida la namna hii ambalo litatoka mara nne kwa mwaka, pia tumeweza kuwa na midahalo mbalimbali ya wazi ya kuelimisha juu ya masuala ya Harusi na ndoa” alisema Hassanali.

Akizungumzia kuhusu muitikio wa watu kuja kutembela maonyesho hayo, Mustafa Hassanali alisema kuwa “kwa mwaka huu, namba ya washiriki imeongezeka zaidi ya ile ya mwaka  jana, huku watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya pia inaongezeka siku hadi siku, jana walikuwa wachache, na hii ilitokana na kuwa jana ilikuwa ni siku ya kazi, ila leo kwakweli tumepokea watu wengi sana, na bado tunawaomba watu wajitokeze kwa wingi kwa siku ya kesho ambao ndo tunafunga rasmi maonyesho haya.” Alimalizia kuzungumza Hassanali.

Hii ni mara ya pili kwa maonyesho haya ya Harusi kufanyika nchini, huku yakiwa na matarajio ya kuishirikisha mikoa mingi zaidi nchini kwa miaka ijayo, tofauti na mwaka huu ambapo mikoa ya Arusha, Zanzibar na Dar es salaam tu ndio iliyoshiriki.

Kwa maelezo zaidi tembelea www.harusitradefair.com


Mfaume Shaban
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road,   Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel :  +255 (0)22 266 8555
Mobile :  +255 (0)655 501 526
Mail : media@mustafahassanali.net
Web : www.mustafahassanali.net
www.swahilifashionweek.com
www.harusitradefair.com
www.twende.info

No comments: