Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
RASIMU ya Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba wa mwaka 2011 imeendelea kupata upinzani mkali huku Chadema kikijipanga kuandamana katika mikoa kumi na NCCR-Mageuzi ikiamua kutinga bungeni mjini Dodoma leo kuwashawishi wabunge kuukataa muswada huo.
Tayari mjadala wa rasimu hiyo umeibua hali ya wasiwasi nchini, huku Rais Jakaya Kikwete akitumia mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliomalizika mjini Dodoma juzi, kueleza kuwa muswada huo siyo Katiba bali ni njia kuelekea uundwaji katiba.
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia, alisema jana kuwa ameandaa tamko la chama hicho kuhusu sababu za msingi za kupinga muswada huo na nakala zake zitakwenda kwa Rais Kikwete, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu.
Kwa mujibu wa Mbatia, nakala ya tamko hilo litafikishwa pia kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, huku akitahadharisha, Muswada huo utaivuruga nchi bila sababu za msingi.
Mbatia Alisema: "Kesho (leo) tutapiga kambi mjini Dodoma, kutakuwa na timu maalumu ya NCCR Mageuzi kuwashawishi wabunge kuukataa muswada huo." Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi alisema muswada huo umezuia mambo nyeti na msingi kwa taifa ikiwamo Muungano na mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, wakati tayari Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 imeyapindua.
Akipitia baadhi ya vifungu nyeti vya muungano katika katiba hiyo ya Zanzibar na ya Muungano, Mbatia alisema mabadiliko yaliyofanyika visiwani yamegusa mpaka mamlaka ya Rais wa Muungano na kunyang'anya mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 24 (3) cha Katiba hiyo.
"Leo muswada unasema tusiguse mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, wakati Katiba ya Zanzibar imekwishayapindua, wanasema tusiguse muungano wakati tayari Zanzibar kuna nchi mbili," alisisitiza.
"Kwa katiba ya sasa ya Zanzibar, Kikwete siyo Rais wa Jamhuri ya Muungano bali ni Rais wa Shirikisho. Kule Zanzibar pia hakuna tena Serikali ya Mapinduzi bali kuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa,"aliongeza.
Alifafanua kwamba ili kupata katiba mpya ni vyema mchakato ukaanzia kwenye marekebisho ya Ibara ya 98 ya katiba iliyopo ambayo itakuwa mhimili wa msingi wa harakati zote za kupata Katiba mpya.
Chadema
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wabunge wa chama hicho wataongoza maandamano yatakayofanyika Aprili 16 mwaka huu katika mikoa 10.
Mkuu wa Operesheni hiyo ya Chadema Benson Kigaila, alisema maandamano hayo yamelenga kuishinikiza Serikali kutekeleza mambo matatu kabla ya kufikia hatua ya kuandikwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Chadema imeona Serikali ya CCM haitaki kutekeleza jukumu la kuandika Katiba mpya, tunakwenda kuandamana katika mikoa kumi ili kuwaunganisha Watanzania na kushinikiza mambo makuu matatu,” alifafanua Kigaila.
Alitaja mambo hayo kuwa ni kuitaka Serikali kubadili rasimu ya muswada huo kwa kuzingatia maoni ya wadau badala ya timu ya watu wachache kwa maslahi yao, kutoa muda kwa wananchi kushauriana na kujadiliana kabla ya kufika bungeni na muswada kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili kuwezesha Watanzania kuelewa na kuujadili kwa kina.

Kigaila aliweka bayana kwamba, rasimu hiyo ambayo tayari imekwishawasilishwa bungeni ina upungufu mkubwa likiwamo la kuvunja katiba iliyopo kwa kuwanyima Watanzania fursa ya kudai haki yao mahakamani kama wajumbe wa tume watakiuka haki katika utendaji wao.
Aliongeza kwamba rasimu hiyo pia imewapora haki wananchi wa Tanzania mamlaka ya kuamua utawala wanaoutaka kwa kuwanyima fursa ya kuandika katiba mpya ambayo kwa sasa imeachiwa kwa wanachama watatu wa CCM.
Kigaila alitaja timu za viongozi wa maandamano hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe (Mbeya), Dk Willbrod Slaa ataongoza Mkoa wa Tabora, Arusha yataongozwa na Naibu Katibu wa Chadema Tanzania Bara, Zitto Kabwe akiongozana na Profesa Abdallah Safari aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni.
Sahringon yajitosa
Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania (Sahringon), umeitaka Serikali kuongeza siku za kutoa maoni kuhusu Muswada mpya wa Sheria wa marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 badala ya siku tatu za sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Taifa wa mtandao huo, Martina Kabisama, alisema siku tatu ni chache kwa wananchi kupata fursa ya kutoa maoni yao na kwamba wananchi wengi watashindwa kufikiwa.
Kabisama aliweka bayana kuwa, Serikali kutoa siku tatu za kukusanya maoni kuhusu marekebisho hayo, ambazo tayari zimekwisha ni uonevu kwa wananchi.
Wataka Werema, Kombani wajiuzulu
Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema wametakiwa kujiuzulu baada ya kutofautiana na Rais Kikwete kuhusu kuwapo kwa Katiba mpya.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na washiriki wa Mdahalo wa kujadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Chriss Maina, alisema kwa nchi zinazofuata utawala bora, viongozi hao wangekwishajiuzulu baaada ya Rais kutoa muswada wa sheria hiyo. Viongozi hao kwa nyakati tofauti waliwahi kusema kwamba Katiba mpya haitatengenezwa kwa sababu ya gharama kubwa na kuwa iliyopo hivi sasa bado inafaa.
Profesa Maina ambaye alikuwa akitoa maada ya ‘Je ,mchakato unaopendekezwa utazaa Katiba inayotokana na matakwa ya wananchi’, alisema hayo baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu viongozi hao kuendelea na nyadhifa zao licha ya kutofautiana na Rais.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment