Kuna uhusiano hai na mfu. Ni wakati wako kupima na kuamua. Unatakiwa kujua kwamba haipendezi kuachana lakini si jambo jema kutumia muda mwingi kutatua migogoro badala ya kupanga maendeleo ya kimaisha na kuboresha penzi.
Uhusiano ambao unatawaliwa na migogoro kila kukicha huo ni mfu. Penzi lenye amani na upendo unaopimika kwa fikra, hutengeneza muunganiko hai wa wawili walioamua kupendana. Linapokereketa huzaa maumivu ya hisia.
Hili si mara yangu ya kwanza kulisema. Ni vyema mtu anapoamua kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi awe amejiandaa kupenda, kuheshimu, kulinda, kunyenyekea na kadhalika.
Wewe unaweza kuwa mtu tu duniani. Ukijitazama thamani yako ni ndogo, usipokuwepo ni familia yako tu ndiyo inayoweza kubaini upungufu. Dunia haitatetereka kwa namna yoyote ile. Ukitembea ni mwepesi na unapigwa vikumbo na wanaojiona wana mbavu nene kuliko wewe.
Pamoja na yote hayo, ndani ya ulimwengu wa kimapenzi wewe ni dunia ya mwenzi wako. Vivutio vyote unavyoviona ulimwenguni haviwezi kumpa amani ikiwa wewe hujataka. Tabasamu lako kwake hujenga utulivu wa moyo wake na kuona siku za kuishi zimeongezeka, kwa hiyo ni vyema kuheshimu.
UNAHITAJI MWENZI WA KUFA NA KUZIKANA?
Bila shaka jibu ni ndiyo. Nimeshakupa pointi tano za kufanyia kazi. Bado kuna vipengele ambavyo leo tunavimalizia.
Awali ya yote nilikutaka utambue “Nani Mwenzi wa Maisha” na baada ya hapo ujiridhishe kujua “Nani Mwenzi wa Maisha Yako”. Nilikutaka “Ujenge Imani” katika kumpata yule wa kweli, ukiamini kwamba hakuna linaloshindikana.
Wiki iliyopita nilikutaka ujiulize, “Anakukubali?”, pia utambue “Thamani Binafsi”, yako wewe na yake. Je, ana sifa unazozihitaji? Nilikusisitiza usithubutu kuingia kwa kulazimishwa au kujilazimisha.
MAWASILIANO
Ni nguzo kuu ya uhusiano. Ikiimarishwa huchochea amani ya kudumu lakini kinyume chake ni kichocheo cha wapenzi kuachana. Je, mwenzi wako ana lugha inayokufanya uelewane naye? Sauti yake akiwa mtaani itofautiane na ile ambayo anaitumia chumbani akiwa na wewe.
Pengine ana kawaida ya kutoa majibu ya mkato unapokuwa unazungumza naye. Kimsingi kama hana mawasiliano mazuri, ni busara umtilie shaka mapema, kwani inawezekana akawa msumbufu baadaye.
ANAKIRI MAKOSA?
Hii ni kanuni nzuri mno kwenye mapenzi. Anatakiwa kutambua makosa yake haraka na kutafuta njia ya kusuluhisha. Akijielewa kwamba amekosea halafu akakaa kimya hutoa ishara mbaya mbele ya safari.
Kama hakubali makosa yake, maana yake ni mbishi, kwa hiyo hilo ni doa.
ANAUNGAMA?
Kiingereza kinatawala sehemu kubwa ya mawasiliano ya Watanzania, kwa hiyo akiona kama akisema samahani ataonekana ni wa kienyeji, basi aseme ‘I am sorry’. Hii ni baada ya kutambua makosa na anapoomba msamaha amaanishe kutoka moyoni.
ANAJISHUSHA UKIWA NA JAZBA?
Ni kanuni ya mapenzi kwamba mwenzako akinuna, wewe jishushe ili mpate muafaka. Nyote mkigoma mtafika saa ngapi? Ni alama nzuri endapo utagundua kuwa mwenzi wako huwa anajishusha kila anapoona umekasirika.
ANASHABIKIA YANAYOKUKWAZA?
Inafundishwa kwamba rafiki wa rafiki yako ni rafiki yako. Adui wa rafiki yako ni adui yako. Rafiki wa adui yako ni adui yako. Adui wa adui yako ni rafiki yako. Falsafa hii ikupe somo kwamba mwenzi wako hatakiwi kupenda yale ambayo unayachukia.
Haikubaliki mtu ambaye hana jema kwa mwenzi wako, wewe umfanye rafiki. Fikiria upande wako kwamba kuna mtu anakula yamini kukumaliza, halafu ugundue kwamba mpenzi wako huwa anaketi naye na kuzungumza kwa kugongeshana mikono. Lazima aheshimu hisia zako.
ANABEBA YANAYOKUHUSU?
Unapokuwa naye anakuonesha mapenzi ya dhati. Hukasiriki unapokuwa naye. Hakukaripii na anakufanya wewe ni bora. Anakusifia kwamba ni mzuri na anakueleza kwa hisia namna anavyokukubali. Huyo anafaa.
ANADHIBITI SAUTI?
Hata kama mmegombana, anapaswa kulinda sauti yake. Je, anatumia hekima kumaliza tofauti zenu? Kama ndiyo, unangoja nini? Huyo ndiye mwenzi wako wa kufa na kuzikana.

No comments:
Post a Comment