ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 17, 2011

Aua wazazi wake kwa mapanga

MKAZI wa Kijiji cha Ngimu wilayani Singida vijijini anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma ya kuwaua wazazi wake kwa kuwakatakata mapanga.Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi, Bi. Celina Kaluba kijana huyo, Rymond  Erasto (26) aliyemuua baba yake Erasto Kilakuro (78) na mama yake Frida Dule (57).

Bi. Kaluba alisema katika tukio hilo lililotokea jana kijijini hapo 
Kitongoji cha Misuna Mei 15, 2011 majira ya saa 1:45 usiku mtuhumiwa pia alimkata panga na kumjeruhi vibaya mpwa wake, Esta Huruma (3) aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.


Bi. Kaluba alisema kwa mujibu wa maelezo ya kaka wa Raymond, Bw. Epata Erasto (40), kuwa mtuhumiwa anayesadikiwa kurukwa na akili aliondoka ghafla nyumbani kwa baba yake akiwa na panga na kisu kuelekea nyumbani kwa kaka yake.

Mtuhumiwa huyo alibaini kuwa baba yake alikuwa anamfuata nyuma, na alipofika eneo hilo alikabiliana na kaka yake ambaye alimwona na kisu na kukimbia.

Baada ya kumkosa kama yake, ilimpa mwanya mtuhumiwa kumrudia baba yake na kumkata panga mara tatu kichwani akafariki dunia na kisha kuingia ndani na kumtaka mama yake mzazi panga kichwani na begani. 

Kama vile haitoshi kijana huyo alimvamia mtoto mdogo anayeishi na bibi yake na kumkata panga kidole cha mkono wa kulia, kichwani na tumboni na kumsababishia majeraha makubwa. 

Kamanda Kaluba alisema kuwa majirani walijaa na kuizingira nyumba hiyo, lakini kila mara walitishwa na kufukuzwa na kujana huyo na kubaki wakikimbia huku na huko, hadi Raymond alipotupa panga lake na kisu, kisha kukamatwa. 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Robert Salimu alikiri kupokea 
maiti hizo na majeruhi moja ambaye hali yake ni mbaya majira ya saa 8:45 usiku wa kuamkia jana.


CHANZO:MAJIRA

No comments: