Advertisements

Tuesday, May 31, 2011

Blatter: Mambo 'shwari' Fifa-BBC

Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la Soka Duniani Sepp Blatter amesisitiza kuwa Fifa haiko kwenye msukosuko, licha ya "pigo kubwa" kwa sifa yake kutokana na madai ya ufisadi.
"hakuna msukosuko kwenye soka, ni matatizo madogo madogo," alisema Blatter.
Blatter alipuuza maoni, kutoka kwa baadhi ya wadau ikiwemo serikali ya Uingereza, kwamba uchaguzi wa urais wa Jumatano ambao yeye ni mgombea pekee uahirishwe.

"wakati serikali zinapojaribu kuingilia kati, basi kuna tatizo," alisema.
"nafikiri Fifa iko imara sana kiasi cha kwamba tunaweza kushughulikia matatizo yetu bila usaidizi."
Kwa jambo lisilo la kawaida, Blatter aliwahutubia waandishi wa habari akiwa peke yake mjini Zurich na kuonyesha ukakamavu licha ya utata unaozunguka shirikisho lake.
Lakini alimaliza mkutano huo kwa majibizano na mwandishi wa habari wa Ujerumani na hasa akizungumzia wakati yeye mwenyewe alipokuwa mwandishi, akilalamikia kuhusu ukosefu wa "nidhamu" kutoka kwa baadhi ya waandishi wa habari, alionya : "hatuko sokoni hapa;tuko katika jengo la Fifa."

No comments: