ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 4, 2011

Dawa ya Babu yazidi kukubalika

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Medicinal Plant (TMF) imetoa taarifa ya utafiti wake na kusema dawa ya mchungaji Ambilikile Mwasapila inafaa kutibu magonjwa mbalimbali.
Taasisi hiyo imetoa taarifa hiyo baada ya kufanya utafiti katika kijiji cha Samunge-Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro nyumbani kwa Mwaisapila.
Utafiti huo ulifanywa na wataalamu kutoka katika taasisi hiyo, ambao walikaa Samunge kuanzia Januari mpaka Februari mwaka huu na kubaini kuwa tiba hiyo inatibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, pumu, shinikizo la damu na mengineyo.

Alisema walitafiti kwa kukusanya maoni kutoka kwa wakazi wa kijiji hicho pamoja na wao wenyewe kutazama mazingira ya eneo hilo.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa TMF, Marwa Gonzaga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akimtambulisha Mganga wa jadi kutoka kijiji cha Nyamwilolelwa Ingombe wilayani Ilemela, mkoani Mwanza, Mhangwa Kapeji, ambaye anatoa tiba inayoonekana kufanana na ile ya Babu.
Hata hivyo, alisema hawakupata ushirikiano wa Mwasapila kutokana na imani yake ndipo Machi walipohamia Ilemela kwa Kipeji.
Alisema wakati wakiendelea na utafiti huo walibaini kuwa tiba hiyo ni mchanganyiko wa mizizi ya miti shamba ya aina mbili ambayo ni ule anaoutumia Babu, kwa jina la kisayansi unaitwa Carissa Spinarum na kwa lugha ya Kisukuma unaitwa Mulo na mti mwingine umefahamika kwa jina la kisukuma la Ntuntwa ndio inapatikana tiba hiyo ya magonjwa sugu.
Alifafanua kuwa watoa tiba hao wote wawili wanatumia mti wa aina moja ambao ni Carissa Spinarum.
CHANZO: NIPASHE

No comments: