Wanajeshi wa Israil wamefyatua risasi dhidi ya makundi ya waandamanaji kwenye mipaka ya Libnan na Syria.

Taarifa zinasema kuwa watu kama 8 wameuwawa.
Maelfu ya Wapalestina na watu wanaowaunga mkono kutoka Libnan na Syria, waliandamana kwenye mipaka.
Walipiga kelele "tutarudi Palestina", na wengine walirusha mawe.
Na kwenye mpaka wa Syria, baadhi ya waandamanaji walivunja seng'enge na kuingia katika eneo linalokaliwa na Israil la milima ya Golan.
Maandamano hayo yamefanywa kukumbuka siku ya kuundwa taifa la Israil, mwaka wa 1948; siku ambayo Wapalestina wanaita "nakba" au janga.
Jeshi la Israil limeishutumu Syria kuandaa ghasia hizo, ili kusahaulisha ulimwengu ukandamiizi unaofanywa kuzima upinzani Syria kwenyewe.
Na wanajeshi wa Israil wamepambana na waandamanaji huko GAZA na ufukwe wa magharibi wa mto Jordan.
Huko Gaza, inaarifiwa kuwa watu kama 15 wamejeruhiwa na bunduki za rashasha na vifaru.
Katika mji wa Ramallah, kwenye ufukwe wa magharibi, mapambano yaliendelea kwa saa kadha, huku wanajeshi wa Israil wakifyatua gesi ya kutoza machozi na risasi za mpira, dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakirusha mawe.
No comments:
Post a Comment