Kikosi cha Simba Kikikaguliwa na Afisa Ubalozi Suleimani Saleh kulia kwake ni Mh:Mshamu Abdullah,
Afisa Ubalozi akikikagua kikosi cha Yanga
Mechi ya watani wajaji ambayo imejichukulia umaarufu mkubwa kwa wachezaji na mashabiki wa pande zote mbili Ughaibuni,kwa mara ya kwanza mwaka huu watacheza nje ya DC.
Homa na matambiano ndivyo vinavyotawala sasa miongoni mwa wachezaji na mashabiki,wachezaji na mashabiki wa Simba na Yanga wataanza kuingia Columbus,OH,kuanzia Alhamisi May 26,Jioni wachezaji kutoka DC na Mikoa mingine wanatarajiwa kuunda timu zao imara kwa ajili ya mpambano huo wa kukata na shoka unaosubiliwa kwa hamu na wakazi wa Columbus,OH na US nzima ambao watakuja mahususi kwenye Bash la Wabongo litakaloanza rasmi Ijumaa May 27,2011 mjini hapo.
Wachezaji na mashabiki wa Simba wamesema safari hii hawakubali kufungwa na Yanga,wengi walisikika wakisema uteja sasa basi,Timu kepteni wa Simba Vincent ameomba na kusisitiza wachezaji waliopo OH na mikoni fanyeni mazoezi ya kutosha mechi hii na Yanga si lelemama ni mechi ngumu na inataka uwe fiti.
Mechi hii itakua ni mechi ya kwanza mwaka huu kuzikutanisha timu hizi mechi ya mwisho Yanga waliibanjua Simba kwa bao 3-2 mabao ya Yanga yalifungwa na Ebra ambae mechi hiyo alikua mwiba kwa mahasimu hao wa Msimbazi.
Mechi ya marudiano itachezewa DC mwishoni mwa September wakati wa sherehe za miaka 50 ya Uhuru.
No comments:
Post a Comment