ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 18, 2011

Museveni asema hataruhusu maandamano.-VOA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alipokula kiapo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alipokula kiapo
Rais Yoweri Museveni apinga maandamano nchini Uganda baada ya wiki kadhaa za maandamano.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hataruhusu maandamano nchini humo  kuendelea baada ya wiki kadhaa za maandamano dhidi ya  serikali.
Bw. Museveni alisema hayo katika taarifa ya maandishi jumanne kwamba atatumia kila kipengele cha sheria kumaliza kile alichokiita uhalifu huu. Aliwalaumu polisi na mahakama kuwa wapole  mno na  kusema kwamba kuna udhaifu katika sheria ambayo inaruhusu utovu wa nidhamu kuwepo.
Rais huyo pia alishutumu vyombo vya habari vya nyumbani na vya kimataifa kwa kushangilia kile alichokiita watu wasio makini ambao ni maadui wa mafanikio ya uponyaji ya Uganda.

No comments: