Tuesday, May 3, 2011

Shukurani za dhati

Ndugu wanajumuia........
Kwa niaba ya New England Umoja Foundation Inc, tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa mahudhurio yenu katika Maonyesho ya Mavazi ya Ki-Tanzania (Fashion show) yaliyofanyika Jumamosi iliyopita pale Leominster MA. Shughuli ilifana sana na tulifanikiwa vizuri mno.
Tunawashukuru kwa upendo na umoja mliouonyesha, kwani bila kujitolea
kwenu tusingelifanikiwa.Tunawaomba muendelee na moyo huo wa upendo, hasa katika shughuli zetu zote zinazokuja.
Jumamosi mvua iliyesha karibu siku nzima kuanzia asubuhi, mpaka Jumapili asubuhi, lakini nyinyi ndugu zetu hamkujali hilo. Milijitoa mhanga kuiunga mkono Jumuia yetu katika jitihada zake za kudumisha Umoja wa wa-Tanzania huku Ugenini, na pia katika hamasa za kuchangia mfuko wa kuadhimisha miaka 10 ya New England Umoja Jumapili July 3, 2011, palepale Camp Keewanee, Greenfield Massachusetts.
Tunapenda pia kuishukuru "Special Event Committee", (moja ya kamati za N.E.Umoja Foundation) chini ya Mwenyekiti wake Abdul Latif Maalim (-Tiff), kwa ushirikiano wao, na kazi nzuri waliyoifanya. Tunamshukuru Siraji Mfangavo kwa kujitolea Vyombo vyake nya Muziki wa kisasa, Kamati ya Chakula na wakina mama wote mliojitolea kwa hali na mali kuhakikisha kuwa kila mtu anakula na kushiba. Asanteni sana.
Vilevile tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa Ma DJ'S  wetu RichiMaka, Masudi, na vile vile bwana "Vijimambo", D.J Luka kwa kujitolea kwao, na kwa kazi nzuri waliyoifanya. Tunaamini kila mmoja wenu aliburudika kwa umahiri wao!.
Mwisho kabisa, tunamshukuu Mama Mitindo mwenyewe, Bi Asia Idarous Kwa Mambo "tisa" aliyotuonyesha. Mambo "kumi" yatakuwa JULY 3rd 2011atakapovunja "Jungu" kwa Show kabambe na ya aina yake!. Jiandaeni na "Fungeni mikanda, misuli kuchanika".
Kwa wale watakao kuwa na hamu ya kungalia picha tembelea www.newenglandumoja.net
Asanteni sana jamani!


salum salum,
Katibu,
New England Umoja Foundation, Inc.


salum salum

No comments: