
Mkuu wa IMF Dominique strauss-Kahn (katikati) akitolewa katika kituo cha polisi mjini New York juzi
MKUU wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF), Dominique Strauss Kahn amefikishwa mahakamani mjini New York kwa madai ya matumizi ya nguvu kushinikiza kitendo kumwingilia kimwili mhudumu wa chumba katika hoteli moja ya kifahari.
Kahn amefikishwa mahakamani ambapo amekana mashtaka yote dhidi yake na kwa mujibu wa wakili wake, mteja wake alikabidhi nguo zake kwa ajili ya uchunguzi wa DNA.
Wakili huyo, William Taylor alisema mkuu huyo wa shirika la IMF alikanusha madai hayo ya kumshambulia mwanamke huyo kwa nia ya kufanya nae mapenzi pamoja na jaribio la kumbaka.
Polisi mjini New York ilisema kuwa Kahn hana haki ya kidiplomasia kumzuia asishtakiwe na kwamba iwapo atathibitishwa kuwa na hati, anaweza kufungwa miaka 15 hadi 20 jela.
IMF imemtaja John Lipsky kuwa kaimu mkurugenzi mkuu na kusema kuwa Nemat Shafik, naibu mkurugenzi mkuu ambaye anahusika na usimamizi wa kazi za IMF katika mataifa kadhaa ya Ulaya, atahudhuria mkutano wa jana Jumatatu mjini Brussels badala ya Strauss-Kahn.
AFP
No comments:
Post a Comment