ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 4, 2011

The Susan G. Komen Global Race for the Cure®

Saturday, June 4 · 7:00am - 

Tunafanya kazi pamoja, tunakutana katika shughuli za pamoja na tunashereheka kwa pamoja. Kwa nini tusifanye jambo muhimu kwa pamoja, kama vile kusaidia kuangamiza ugonjwa wa saratani ya maziwa (breast cancer).
Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa kusherehekea miaka 10 tangu mwenzetu, mama yetu, dada yetu, shangazi yetu Rehema Barksdale kupona saratani ya ziwa (Breast cancer survivor). Anatupa moyo sisi wote, familia yake na marafiki. Hivyo katika kumuunga mkono kwa mwamko wake kwetu sote, Ubalozi wa Tanzania na familia yake wanatayarisha kikundi maalum cha Watanzania, Team Tanzania, kushiriki katika matembezi ya “Susan G. Komen Global Race for the Cure”. Tunategemea kuwa utajiunga nasi.

Lengo kubwa la kikundi hiki ni:
·         kuleta uelewa wa saratani ya maziwa katika jumuiya yetu ya watanzania hapa DC metro; 
·         kuwaunga mkono wanawake walioweza kutibiwa na kupona na matatizo hayo; na
·         kuchangisha fedha zitakazotumika katika utafiti, elimu na huduma katika matibabu ya saratani ya maziwa.

Tarehe 4 mwezi wa Juni, maelfu ya watu watakutana katika uwanja wa National Mall hapa Washington DC kutoa mchango wao katika juhudi za dunia kupiga vita na kuuangamiza ugonjwa huu. Bila ya matibabu, inasadikiwa kuwa kiasi cha watu milioni 25 duniani wataonekana kuwa na saratani ya maziwa;  na katika miaka 25 ijayo, kiasi cha watu milioni 10 watafariki kutokana na ugonjwa huu. Huu ni wakati mzuri kutumia fursa hii kutoa mchango wetu katika jambo hili. Kwa pamoja tutaweza kuuangamiza ugonjwa huu.

Basi tuanze leo. Jiunge na Team Tanzania kwa kubofya hapa

Kama utashindwa kutembea au kukimbia nasi uwanjani siku ya matembezi hayo, tuunge mkono kwa kutoa mchango wako (haotolipishwa kodi) kwa Team Tanzania.
Kama una swali lolote usisite kuwasiliana nasi kwa kutuma email kwa: Nelleta Kassembe email: nelleta.kassembe@gmail.com au kupiga simu namba 240-393-6954; au kumpigia Joyce Kassembe, email: jkapea@gmail.com simu namba 240-646-2405.

Vyovyote  utakavyoamua kushiriki, cha muhimu ni kwamba unatuunga mkono katika juhudi za dunia kupiga vita na kuuangamiza saratani ya maziwa. Asanteni

Ada ya kujiandikisha kwa sasa ni $35 kwa mtu mzima na $20 kwa mtoto (miaka 5 – 12). Baada ya tarehe 15 April, itapanda kuwa $40 kwa mtu mzima na $25 kwa mtoto (miaka 5 – 12). Mara utakapojiandikisha utatumiwa T-shirt na karatasi yenye namba ambayo utaivaa wakati ya kutembea. 

No comments: