ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 4, 2011

Wanasheria nchini Uganda waandamana kupinga ukatili wa polisi-VOA

Waandanmanaji wakiwa katika karandinga la Polisi.
Wanasheria waamua kuandamana Uganda kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu
Wanasheria  nchini Uganda wanapinga matumizi ya nguvu ya serikali dhidi ya waandamanaji wanaolalamikia bei kubwa za chakula  na mafuta.
Zaidi  ya wanasheria100 walikusanyika nje ya  mahakama kuu ya Uganda Jumatano ambapo waliwalaani maafisa wa usalama na kuanza kile walichokiita mgomo wa siku tatu.

Polisi nchini Uganda wametumia gesi ya machozi, risasi za mpira na risasi za moto ili kuvunja mandamano kadhaa katika mji mkuu Kampala katika mwezi mmoja  uliopita. Umoja
Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye anaongoza maandamano hayo amekamatwa mara nne. Wiki iliyopita, polisi walivunja dirisha la gari lake na walimwagia gesi ya machozi kabla ya kumtia  ndani.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema serikali yake haitavumilia maandamano na ametetea hatua za  polisi. Analaumu kuwa hali kupanda kwa gharama za maisha nchini Uganda kunatokana na ukame na kupanda kwa bei za mafuta duniani.
Wanasheria wanataka uchunguzi ufanywe kuhusiana na jaji  Justine Atukwasa, ambaye wanasema hakuwa muadilifu  katika kesi ya  Besigye.
Besigye anaongoza upinzani nchini Uganda kwa zaidi ya muongo mmoja. Ameshindwa mara tatu katika uchaguzi wa urais dhidi ya bwana Museveni, ambaye ameiongoza Uganda tangu mwaka 1986.

No comments: